ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 16, 2013

MKAZI WA BUHEMBA ANASWA NA VIPANDE 10 VYA MENO YA TEMBO VYA THAMANI YA MILIONI 23.2 AKISAFIRISHA JIJINI MWANZA.

 MKAZI wa Kijiji cha Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara Yohana Jackison (27) amekamatwa na Askari Polisi wa dolia akiwa na vipande 10 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 23.2 Jijini Mwanza.
Gunia lililokamatwa na nyaraka hizo za serikali (meno ya Tembo).

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Evarist Mangu jana alieleza kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisafirisha meno ya tembo kutoka kijiji cha Buhemba kuja Jijini Mwanza alikamatwa na askari wa dolia katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Buzuruga majira ya saa 3:15 asubuhi kwenye kilichopo eneo la Nyakato baada ya kushitukiwa na askari hao.
Kamanda Mangu alisema kwamba baada ya kushuka kwenye basi dogo mali ya Kampuni ya JOHANVIA Express linalofanya safari zake kati ya Butiama na Mwanza akiwa ameficha vipande vya meno hayo ya Tembo kwenye gunia la mkaa ambapo baada ya kutelemka na kuonyesha wasiwasi ndipo askari hao waliamua kumsimamisha.
Vipande vya meno ya Tembo vikikaguliwa mara baada ya kutolewa kwenye gunia.


Yohana Jackison (27)

 “Baada ya kumsimamisha walimhoji kabla ya kuanza kumpekuwa na ndipo walipogundua kuwa katika gunia la mkaa kunavitu vingine na walipozidi kuumwaga mkaa walikuta kifurushi kikiwa kimefungwa ndani yake kukiwa na vipande 10 vya meno ya Tembo ikiwa ni Nyara za Serikali ” alisema Kamanda Mangu na kuongeza kuwa.
  
Gunia la mkaa ambamo kulikuwa na fuko la pembe za ndovu.

Mtuhumiwa Yohana Jackison (27) akivirejesha vipande vya ndovu kwenye fuko lake alilolificha ndani ya mkaa.


 Baada ya askari hao kuona vipande hivyo waliendelea kumshikilia na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Kati ili kumhoji zaidi na kuwatafuta Maafisa wa wanyama pori wa Idara ya Maliasili ili kufanya utambuzi zaidi wa meno hayo ambapo ilithibitishwa  kuwa ni meno ya tembo.
  
 Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia ujangili Mikoa ya Kanda ya Ziwa Benjamin Kijika alisema kwamba vipande hivyo ni vya tembo wawili na ni meno manne ambavyo vilikatwa vipande vipande na kutoka 10 ili kumrahisishia katika ubebaji wake na tembo hao waliuwawa kwa Ujangili.
“Vitendo vya ujangiri ambavyo vimekuwa vikishika kasi ya kushamili kwenye maeneo mbalimbali ya Hifadhi za Mbuga za Wanyama Pori na maeneo tengefu hapa nchini kwa sasa vimepewa kipaumbele kwa kuwasaka wahalifu na majangiri na  watu ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya meno ya tembo hapa nchini” alisema Kijika.
Kamanda Kijika amelipongeza Jeshi la Polisi maeneo yote ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchini kwa kuweka kipaumbele kupambana na wahalifu wakiwemo majangili wa wanyama pori ambao ni rasilimali kubwa ya Taifa  na kuitendea haki nchi yetu na wanyama pori kwa kuendelea kukuza sekta ya utalii ambayo imekuwa ikituingizi mapato ya fedha za kigeni.
Kamanda huyo amewataka wananchi pia kuanza kuwafichua majangiri kwa kuwataja na kutoa taarifa za siri kwa wakuu wa polisi wa Wilaya na Mikoa yote ili kuwakamata kabla ya kufanya uhalifu wa kuuwa wanyama pori na hata kufanya ujambazi wa unyang’anyi wa kutumia silaha ili kudhibiti wimbi la vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.