Mbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kuwa maadili ya uongozi na utawala bora, vinatikiswa kama siyo kuyumbishwa. Aliwataka wananchi kuhakikisha misingi ya taifa inarekebika kupitia marekebisho ya katiba mpya.
Mnyika alisema kuwa katika kupitisha maoni ya katiba, wanataka haki, uwazi na usawa katika masuala ya madini na rasilimali za nchi ambazo kimsingi zinapaswa kutajwa kwenye katiba. Tunataka Katiba pia impunguzie rais madaraka, alisema.
Alisema gharama za maisha ya wananchi zinazidi kupanda kila kukicha kutokana na rais kuwa na mlimbikano wa madaraka, hivyo kufanya maamuzi bila kutambua kuwa wananchi walio na kima cha chini ndio wanaoumia.
Aidha alisema kuwa anashangazwa na serikali ya CCM inavyokataa mfumo wa serikali tatu kwa madai kuwa,serikali tatu ni gharama kubwa sana kuendesha huku wakisahau baraza kubwa la mawaziri lisilo na meno.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.