|
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la Tigo Mwanza lililopo barabara ya stesheni ambapo tawi hilo lilifungwa kwa muda kupisha ukarabati mkubwa kuendana na mahitaji ya huduma bora na za kisasa. |
|
"Moja kati ya sababu za wawekezaji kukimbilia jijini Mwanza iwe ni shughuli za kibenki, mahoteli au shughuli za mawasiliano: kwanza kupitia sensa ya mwaka jana jiji la Mwanza ni la pili kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya jiji la Dar es salaam, ni jiji la pili kuchangia pato la Taifa.
Na ukisema jiji la Mwanza unazungumzia wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wachimbaji madini na wasafirishaji, hivyo kwa mwekezaji yeyote akishawekeza Dar es salaam fikra zake humtuma kuja kuwekeza Mwanza ambako vilevile shughuli za kiuchumi zinaenda kwa kasi." alisema Konisaga.
|
|
Sehemu ya wafanyakazi wa Tigo tawi la Mwanza wakifuatilia kinachojiri kwa umakini. |
|
Wakuu wa idara mbalimbali Tigo wakifurahia yanayojiri. |
|
Engo na engo.... |
|
"Tulifunga ofisi zetu takribani mwezi mmoja na nusu ili kufanya ukarabati kubadilisha muonekano na pia kuongeza huduma mbalimbali ambazo zitarahisisha shughuli za mawasiliano ya kila siku kwetu sote" Mwangaza Matotola ambaye ni Service Excellence manager wa Tigo |
|
Engagement wa kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kadi maalum ya 'Kipaumbele'. |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, naye alipata fursa ya kukabidhi wateja wa kwanza wa jiji la mwanza kupata kadi maalum ya 'Kipaumbele' na hapa alikuwa akimkabidhi bwana Alan Seif Said. |
|
Jackson Jerry ambaye ni Engagement Specialist wa Tigo akiwa na zawadi ya smart phone ambayo ilikabidhiwa kwa rafiki mkubwa wa Tigo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyanagana jijini Mwanza Baraka Konisaga akimkabidhi Jackson Kabeza zawadi ya smartphone kwa kuwa rafiki mkubwa mfuatiliaji wa Tigo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. |
|
Wananchi wa Kanda ya Ziwa wategemee kupata huduma bora za mawasiliano kutoka Tigo. |
|
Ndani ya tawi hili mteja atapata fursa kuona na kujaribu bidhaa. |
|
Mkuu wa wilaya akiendelea kukagua tawi la Tigo Mwanza. |
|
Mazingira mapya ya ofisi ya Huduma kwa mteja na Tigo tawi la Mwanza. |
|
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wadau wa Tigo juu ya kuridhishwa kwake na ubora wa mazingira ya ofisi za Tigo tawi la Mwanza, kulia ni Retail Operation Manager wa Tigo Charles Sardina. |
|
Wafanyakazi wa Tigo wakishea taarifa. |
|
Picha ya pamoja Wafanyakazi wa Tigo Tawi la Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga. |
WANAOTUKANA KWENYE SIMU KUKIONA
WATU wanaotumia simu za mkononi kutoa lugha za matusi kwa kuongea au kuandika ujumbe mfupi dhidi watumiaji wengine watachukuliwa hatua za kisheria.
Onyo hilo lilitolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, alipozungumza kwenye ufunguzi wa tawi la ofisi ya Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Alisema kumekuwapo na baadhi ya watu wanaotumia vibaya teknolojia ya mawasiliano ya simu kwa kuwatukana wenzao, na bahati nzuri Serikali imehimiza na kufanikisha kwa asilimia kubwa zoezi la usajili wa laini za simu za wateja wa makampuni yote hivyo suala la utambuzi limerahisishwa ambapo hatua kali zitachukuliwa kwa watakao kiuka maadili.
Kwa mujibu wa DC Konisaga, Kampuni ya Tigo ina wajibu wa kuhakikisha inadhibiti hali hiyo kwa wateja wake, kwani kufanya hivyo italeta tija kwa wateja wa kampuni hiyo.
“Kwanza naupongeza sana uongozi wa Kampuni ya Tigo kwa kufungua ofisi hapa jijini Mwanza. Huu ni uwekezaji mzuri sana katika maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Lakini kuna baadhi ya watu wanatumia vibaya mawasiliano ya simu kwa kuwatukana wenzao. Serikali inataka Tigo idhibiti hali hii na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Konisaga.
Kwa upande wao, Meneja Huduma na Ubora wa Kampuni ya Tigo, Mwangaza Matotola, kutoka makao makuu, Jackson Jerry na Operesheni Meneja wa Tigo Mwanza, Charles Sardina, walisema wateja wa kampuni hiyo watanufaika na kadi maalumu za ‘Kipaumbele.’
“Kwa kutambua na kuthamini michango ya wateja wetu, Tigo tumeboresha huduma zetu maradufu, wateja wetu watanufaika na kadi za Kipaumbele, watapata huduma bure kwenye matawi yetu 33 nchi nzima,” alisema Jerry.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.