ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 30, 2015

"WAKATI UCHAGUZI MKUU UKIKARIBIA MAISHA YA WATU WENYE ALBINISIM YAKO HATARINI NCHINI TANZANIA" ASEMA PETER ASH

"Nina ndoto kwamba siku moja nchini Tanzania, watu wenye ulemavu wa ngozi watachukua nafasi yao inayostahiki. Na kwamba siku za ubaguzi dhidi ya watu wenye albinism zitakuwa kumbukumbu iliyofifia" amesema Peter Ash, Muasisi wa Under the SAME SUN (kulia).
Vicky Mtetema (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza na kulia ni Muasisi wa UNDER THE SAME SUN Peter Ash akionesha moja kati ya vipeperushi vya elimu kwa umma kuhusu suala la albinism.
TUKIZUNGUMZIA ukatili kwa watu wenye Albinism duiani, ni matukio mengi yametukia nchini Tanzania tangu mwezi Mei 2013 ikiwa ni pamoja na mauaji na watu kukatwa viungo hadi tukio  la mwisho lililosisimua wengi na kuwabakiza njia panda, lililotokea mnamo tarehe 27 Dec 2014 ambapo mtoto Pendo Emanuel alitekwanyara na watu ambao hawajajulikana hadi leo katika kijiji cha Ndame wilayani Kwimba mkoani Mwanza.


Kwa mujibu wa tafsiri aliyokuwa akiitoa Vick Mtetema kuwasilisha taarifa ya Muasisi wa Shirika la Under The Same Sun ambalo limekuwa likijibidiisha katika kuibua yale yaliyofichika yanayohusu changamoto, manyanyaso na ukatili kwa watu wenye albinism, Bw. Peter Ash, baada ya kufanya ziara kwenye kijiji cha Ndame wilayani humo (Kwimba) na kukutana na mama yake Pendo aitwaye Sofia Juma, amepokea malalamiko toka kwa mama huyo ambaye amelelemika kuwa tangu apate tatizo hakuna kiongozi yeyote wa Kisiasa aliyethubutu kumtembelea kujua hali yake au kutafuta ufumbuzi akiwemo yule wa jimbo lake aliyempigia kura.


Wanahabari kusanyikoni.
"Kwanini hata yule mbunge niliyempigia kura hajawahi kuja kunitembelea kunisikiliza na kujua jinsi mtoto wangu alivyotekwa nyara?"

Hiyo ni hali ambayo imekuwa ikijirudia, Peter Ash akikutana na malalamiko kama hayo pindi anapozitembelea baadhi ya familia zinazokumbana  na masahibu kama hayo yanayohusisha watu wenye ulemavu wa ngozi (wenye albinism).
"Hata familia ya mtoto Karim Kasimu (4) anayeishi na wazazi wake Nyakato jijini Mwanza ambaye pia alinusurika kutekwa nyara tarehe 6 Januari 2015 akiwa karibu na nyumbani kwao, ile familia haijaona kiongozi yoyote wa kisiasa aliyethubutu kutembelea kuona jinsi gani anaweza kuisaidia kushiriki kwa namna moja au nyingine kuwalinda watu wenye albinism" KUMSIKILIZA BOFYA PLAY


Wanahabari kikazi zaidi.
Katika nchini nyingi zenye imani potofu barani Afrika ikiwemo Tanzania inaaminika kuwa magonjwa sugu na hata yale ya kuambukiza kusafishwa kwa kumbaka mtu aliye na ulemavu wa ngozi (albinism). Moja kati ya matukio yaliyotokea ni lile lililotokea mkoani Shinyanga ambapo bintimmoja mwenye alibakwa na watu watano wenye maradhi wadai kujisafisha maradhi. BOFYA PLAY KUSIKILIZA 

AMRI BILA VITENDO NI KAZI BURE.
Hoja imewasilishwa kwa njia ya swali:- Hivi hiyo amri ya kupiga marufuku upigaji ramli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani inatofautiana nini na amri iliyotolewa na Waziri Mkuu mnamo Januari 2009,amri ambayo hata hivyo ilikuja kufutwa tarehe 30 September 2010 mwezi mmoja kabla ya UCHAGUZI MKUU?

Kwa sasa hivi tunaelekea kwenye UCHAGUZI MKUU mwingine, nayo amriimetolewa. Jeh hii amri itakuwa na uzito, itafanya kazi, itatimiza malengo yaliyokusudiwa? BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Mwanahabari Albert G. Sengo akitafakari mara baada ya kutoka chumba cha mkutano na wadau wa Under the same sun uliofanyika katika ukumbi wa Hotel Ryans Bay wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
UMOJA WA MATAIFA WAAMUA KUHUSU WATU WENYE ALBINISM
Zaidi ya matukio 152 ya mauaji yametokea ndani ya kipindi cha miaka 14 nchini Tanzania lakini ni asilimia 5 tu ya kesi zake zimefikishwa mahakamani.

Umoja wa Mataifa umetambua Umuhimu wa kuliangalia hili suala la watu wenye albinism, hali yao na ukatili unaofanywa dhidi yao na sasa umeitenga kuanzia mwaka huu tarehe 13 mwezi JUNI ya kila mwaka kuwa 'SIKU YA ALBINISM DUNIANI'
BOFYA PLAY SIKILIZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.