·
Ben Paul, Grace
Matata waongezeka kwenye burudani, Mrisho Mpoto na Weusi kusindikiza
·
Viingilio shilingi
elfu 15 kwenye vituo na elfu 20 mlangoni
Tamasha la miaka
kumi ya THT litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni,
limekamilisha maandalizi yake na hivyo kuwataka wadau na wapenzi wake wajitokeze
kwa wingi kushuhudia burudani kubwa ya mziki hapa nchini.
THT, ambayo
inasifika kwa kuzalisha wasanii mahiri nchini kama Linah, Barnaba, Mwasiti,
Ditto, Mataluma, Vumi, Beka, Recho, Marlaw, Msami, Makomando na wengine wengi,
imejipanga kutoa burudani kubwa ya mziki kwa mashabiki wake.
Akizungumza kuhusu
maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa THT, Mwita Mwaikenda alisema maandalizi
yanaenda vema na mashabiki wahudhurie kwa wingi kujionea namna kituo hicho kilivyoweza
kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya muziki.
‘Mpaka sasa wasanii
wa THT watakaotoa burudani wako tayari, na kama mnavyojua THT utamaduni wake ni
kupiga muziki kwa kutumia bendi lakini pia wasanii watakaotusindikiza ni kama
Ben Paul, Mrisho Mpoto na Weusi’ alisema Mwita.
Akizungumzia
wadhamini waliojitokeza kwenye shughuli hiyo, Mwita aliwashukuru Mr. Price
waliowavisha wasanii wote, Mziiki.Com ya Spice Afrika walionunua tiketi 500 za
tamasha kwa ajili ya wateja wao, SanMoto Pikipiki waliotoa pikipiki, Tanzania
Fashion and Design Limited, Darling Hair ambao wametoa nywele kwa waimbaji wote
wa kike na Clouds Media Group.
‘Tunatoa shukrani za
dhati kwa wadhamini wetu, kwa kutuunga mkono katika kuadhimisha miaka kumi ya
kuleta mapinduzi katika burudani’ alisema Mwita.
Tiketi za tamasha
zinapatikana maduka ya Robby One Fashion Kinondoni na Sinza, Yahya Boutique
Kinondoni, Born 2 Shine Mwenge, Ofisi za Clouds, Moca City Samora Avenue, City
Sports Lounge, Mr Price na THT Kinondoni.
Kiingilio ni
15,000/- kwenye vituo hivyo na kwa wale wanaotaka za VIP ni 50,000/- na
zinapatikana THT pekee yake.
Siku ya onesho pale
Escape One, mlangoni kiingilio kitakuwa ni Shs 20,000/=.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.