Chama cha mpira wa
kikapu mkoa wa mwanza (MRBA) kupitia kamati ya michezo mkoa wa Mwanza kimetangaza
majina ya viongozi wa muda ambao utakuwa madarakani kwa muda wa miezi mitatu
kuanzia tarehe 01.02.2015.
Lengo kuu la
kutangazwa viongozi hawa pamoja na kuziba nafasi za viongozi waliokuwepo awali,
ni kuwataka viongozi hawa kufanya uchaguzi mkuu sambamba na kuzielekeza klabu
mbalimbali kufanya uchaguzi wa viongozi katika klabu ili waweze kushiriki
uchaguzi ngazi ya mkoa.
Viongozi hawa
wanaziba nafasi za viongozi waliokuwepo awali ambao kwa sasa hawapo kutokana na
sababu mbalimbali.
Uongozi wa awali ulikuwa ni kama ifuatavyo:
11.
Sadoti Mazigo (Mwenyekiti) – alihama
mwanza.
22.
Adam Nyoni (Makamu Mwenyekiti) – alihama
mwanza.
33.
Chikoko (Katibu Mkuu) – alihama mwanza.
44.
Victor Maleko – Katibu msaidizi
55.
Flora Kavavila – Mweka hazina (Alifariki)
66.
Amri
Mohamed – Kamishna wa Makocha.
77.
Twalib Puzo – Kamishna wa Waamuzi.
88.
Diana Deodatus – Kamishna wa wanawake.
99.
Haidary Abdul – Kamishna wa ufundi na
uendeshaji mashindano.
110. Kizito Bahati – Kamishna wa watoto na maendeleo ya mashule.
111. Vincent Shinda – Mchezaji mwakilishi.
Nafasi
zilizozibwa ni wahusika ni wafuatao.
11.
Juvenile Kaiza – Kaimu Mwenyekiti.
22.
Benson Nyasebwa – Kaimu Makamu
Mwenyekiti.
33.
Shomali Almasi – Kaimu Katibu Mkuu.
44.
Vitalis Ndanu – Kaimu M/Hazina
Viongozi hawa
watashirikiana na waliopo katika kuendeleza mpira wa kikapu mkoa wa mwanza.
Imetolewa na:
Kizito Sosho
Bahati
Kaimu Katibu Mkuu
MRBA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.