ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 8, 2022

MABORESHO YA MAPANGO YA AMBONI KUIUNGANISHA TANGA NA ZANZIBAR KIUTALII

 

Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni Mecksadeck Mwambungu akizungumza wakati wa Semina kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George akifuatiwa na Kaimu Meneja  Uhusiano wa Umma NCAA Joyce Mgaya
Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma wa  Mamlaka  NCAA Joyce Mgaya akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George na Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni Mecksadeck Mwambungu
Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma (NCAA) Joyce Mgaya akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George na Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni Mecksadeck Mwambungu
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George akitoa neno wakati wa semina hiyo kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma wa NCAA Joyce Mgaya kulia ni Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni Mecksadeck Mwambungu
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga Burhan Yakub akiuliza jambo wakati wa semina hiyo
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Radio One Mkoa wa Tanga Wiliam Mngazija akiuliza swali katika semina hiyo
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorogoro (NCAA) imeanza mkakati kabambe kwa kuleta Mapinduzi Makubwa ya kiutalii katika Mkoa wa Tanga kupitia Mapango ya Amboni baada ya kueleza dhamira yao ya kutaka kuunganisha utalii unaofanyika kwenye mapango ya Amboni na Visiwani Zanzibar.

Mkakati huo ulitangazwa na Mkuu wa Kanda wa Hifadhi ya Mapango ya Amboni Mecksadeck Mwambungu wakati wa Semina kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

 

Mwambunhu ambaye pia ni Afisa Malikale Amboni kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alisema mkakati huo unakwenda sambamba na kuhakikisha wanafanikisha upatikanaji wa boti ya watalii wanaotoka zanzibar iliwaweze kukaa amboni kwa muda kidogo.

“Kwa kweli mkakati wetu ni kuhakikisha tunaunganisha utalii unaofanywa mapango hayo na Visiwani Zanzibar na tunakusudia kuhakikisha tunafanikisha upatikanaji wa boti kwa lengo la kuwawezesha wakija kwenye mapango hayo wanakaa muda mrefu”Alisema

 

Bw. Mwambungu ameongeza kuwa NCAA wanamkakati wa kuanzisha utalii wa Boarder(mpakani) kwani kuna watu wanatamani kufika Kenya na hawajui watafikaje na kutoka Horohoro mpaka Amboni ni Kilomita 60 hivyo  wanataka kuweka mpango wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha kufika na kufurahia utalii.

 

“Lakini tatu tunataka kuangalia vivutio vya vilivyopo jirani na Tanga tuweze kuviinua vikiwemo Marine Park na eneo la Maji Moto tunaamini tukiviinu vizuri vitaleta tija kubwa”Alisema  

 

Hata hivyo alisema suala lingine ambalo wanalifikiria ni kutaka kuhakikisha kwamba wanaongeza idadi ya watalii kwenye eneo la Mapango ya Amboni na wanaamini kutokana na mikakati walioweka utafanikiwa.

 

“Kwa sasa tunapokea watalii karibia 1000 mpaka 2000 wengi ni wenyeji na wageni ni wachache sana hivyo tunaamini kutokana na maboresho yaliyofanyika ya miundombinu itakuwa ni fursa nzuri kwao kuweza kuongeza idadi hiyo “Alisema

 

Hata hivyo alisema kwamba mpango wao waliokuwa nao kwa sasa ni kuanzisha ulipaji kwa njia ya mtandao na mahitaji muhimu kwa watalii ambapo wanaamini utakuwa na manufaa makubwa.


Awali akizungumza wakati wa semina hiyo Kaimu Meneja  Uhusiano wa Umma wa NCAA, Joyce Mgaya alisema eneo la Mapango ya Amboni limekuwa na simulizi nzuri na ya kuvutia kutokana na kwamba ndani ya mapango kuna eneo ambalo watu wanafanya ibada wa imani tatu tofauti kwa wakati mmoja na wanaweza kuabudu na kuamini sawa kwamba wakienda hapo wanafanya ibada na kuaminiana

“Hivi sasa kuna utandazawazi mkubwa baadhi tunapoteza hamasa ya kupenda simulizi zetu au kupenda vya kwetu na badala yake tunathamini simulizi za nje ..nadhani kwenye mapango kuna mtu anasafiri kutoka nje ya nchi anakuja kufanya tambiko na kuondoka”Alisema


Hata hivyo alisema kwamba wanafikiria kuweka kitanda kwenye mapango ili watu wanaokwenda kutalii eneo hilo waweze kupata eneo la kupumzika usiku na kuweza kusikilizia usiku kunakuwaje.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.