ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 14, 2025

TAKRIBANI SH BILIONI 245 ZAHITAJIKA KUTEKELEZA MPANGO WA USIMAMIZI MAJI-BONDE LA MAJI ZIWA VICTORIA

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Takribani shilingi Bilioni 245 zahitajika kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Maji – BONDE LA ZIWA VICTORIA. Robert Sunday, ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, akizungumza kwenye Jukwaa la Wadau wa Sekta Mtambuka lililofanyika jijini Mwanza, anasema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Maji la Ziwa Victoria, ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ya utunzaji mazingira. Sunday amesema mpango huo unalenga kuboresha matumizi endelevu ya maji, uhifadhi wa vyanzo vya maji, pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli za usafi wa mazingira kwa jamii zinazozunguka bonde hilo. Aidha, amewataka wadau kushirikiana kwa karibu na serikali katika utekelezaji wa mikakati hiyo ili kuhakikisha upatikanaji wa maji salama, usalama wa mazingira na maendeleo ya kijamii na kiuchumi vinaimarika. Tathmini ya Umoja wa Afrika ikishirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika na Shirika la Global Worker Partnership imeonyesha kuwa ili bara la Afrika lifikie malengo endelevu ya kimataifa ifikapo mwaka 2030, zinahitajika dola za Marekani milioni 30 kwa mwaka kwa ajili ya sekta ya maji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment