NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua Mradi wa Dunia wa kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi. Amesisitiza kuwa wizara, taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment