Ni katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa katika dimba la Al Rashid Stadium pale Dubai ambapo timu ya Iran imeibuka na ushindi wa mabao mawili bila majibu dhidi ya Stars.
Wafungaji wa Iran ni washambuliaji Amirhossein Hosseinzadeh dakika ya 17 kwa njia ya penati baada ya beki wa Stars Ibrahim Baka kufanya madhambi ndani ya 18, na Mohhamad Mehdi Mohebi katika dakika ya 28 aliyepokea pande kutoka kwa K. Taheri.
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment