ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 17, 2025

VIDEO;-RC MTANDA AFUNGUKA MAZITO AZINDUA BODI YA NANE YA MAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA NA KUKABIDHI MAGARI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameitaka bodi mpya ya Bonde la ziwa Victoria kusimamia menejimenti ya bonde la ziwa hilo ili iwajibike ipasavyo katika kulinda rasilimali maji kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Mhe. Mtanda ametoa rai hiyo jana tarehe 15 Oktoba, 2025 wakati akizindua bodi ya nane ya bonde hilo pamoja na vitendea kazi (Magari) kwa ajili ya matumizi ya bodi hiyo hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya bonde hilo jijini Mwanza. Mhe. Mtanda amesema katika kutekeleza majukumu yao wana wajibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya taratibu na sheria za matumizi ya rasilimali maji na sio kusubiri mwananchi akosee ndipo wamchukulie hatua hususani wanaochimba visima vya maji. Aidha, Mhe. Mtanda ameishukuru Serikali kwa kutoa Tshs.Bilioni 264.8 mkoani humo katika sekta ya maji ambazo zimetumika kuongeza upatikanaji wa maji mjini vijijini kutoka 58% hadi 85% na kutoka 53% hadi 77% kwa mjini huku akibainisha uwepo wa miradi kadhaa vijijini na mijini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment