ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 5, 2024

KWANINI DAGAA WA MWANZA WAWE NA MCHANGA CBE YAJA NA MAFUNZO BURE KUNUFAISHA WAVUVI & WAJASILIAMALI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Wafanyabiashara wengi wa samaki na dagaa jijini Mwanza wanafanya biashara hiyo kwa mazoea, hawaioni biashara ya samaki na dagaa kama inaweza kuwa kubwa na kuwatoa katika hatua moja ya chini na kuwapeleka hatua nyingine kubwa ya kimaendeleo. Mbinu za biashara ya ni zile zile miaka nenda miaka rudi hali inayopelekea soko kuwa gumu Licha ya kuhifadhiwa maeneo yasiyo na ukavu na ubora, uanikaji na utayarishaji wa bidhaa hususani dagaa bado ni duni ukiathiriwa na vitendea kazi hali inayopelekea bidhaa hizo kuvunda na kuwa na takataka mbalimbali kwani huanikwa maeneo ya miamba, kwenye nyasi, huku wengine wakianika aridhini (mahala ambapo hapajasakafiwa), hali inayopelekea dagaa wengi kuwa na mchanga. Kwa kuyaona yote hayo ikiwa ni baada ya kufanya utafiti maalum, Chuo Cha Elimu Ya Biashara (CBE) kimeamua kuja na mpango wa kutoa elimu kupitia masomo maalum ya kozi za muda mfupi kwa wafanyabiashara wadogo na wajasiliamali mkoani Mwanza ili kuwawezesha wapate matokeo yenye tija katika bishara hiyo ya mazao ya samaki. Jeh Mpango huo umelenga kuwafikia wajasiliamali wangapi? Jeh kuna gharama au masharti yoyote yenye vigezo na sifa vinazozingatiwa hasa ukizingatia wavuvi wengi baadhi yao hawana elimu za viwango vya juu na wengine hawajasoma kabisa? Dr. Robert Galan Mashenene ambaye ni Mkurugenzi wa CBE Campas ya Mwanza anazungumza nasi......... #cbe #samiasuluhuhassan #mwanza

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.