ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 26, 2014

HUYU NDIYE MSHINDI WA NDOVU GOLDEN EXPERIENCE.

Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya pili ya kampeni ya “Ndovu Golden Experience” yakusaka washindi wa kutembelea hifadhi ya Selous. Amandi Kimario mkazi wa Mbezi alishinda katika droo hiyo. Kushoto ni mwakilishi kutoka bodi ya kubahatisha nchini, Humudi Semvua.
NA MWANDISHI WETU
MSHINDI wa pili ya shindano la Ndovu Golden Experience Amand Kimario amewapiga kumbo washiriki wenzake katika shindano hilo na kujinyakulia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Selous mwakani.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt ambao ndio waratibu wa shindano hilo Pamela Kikuli alisema, lengo la kuandaa shindano hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa Watanzania kutembelea hifadhi na kujivunia utalii wao wandani.

Pamela alisema, mshindi huyo amepatikana baada ya kuchezeshwa droo ambapo yeye aliwabwaga wenzake waliojitosa katika shindano hilo, ambapo atatarajiwa kuwana mwenzake ambaye wataongozana katika hifadhi hiyo.

Alisema, kwa kutambua bia yao ya Ndovu inabebwa na nembo ya mnyama Tembo, wanatumia nafasi hiyo kumlinda mnyama huyo kama kampeini yao inavyosema 'Ndovu Defance', ilikunusuru mauaji yake.

"Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania, ila utalii mkubwa unaofanyika hapa Tanzania niwa wageni wa nje, hivyo basi tunaamini kwa kuendeleza kampeini yetu hii ya Ndovu Golden Experience, inayoendeshwa kwa kutumia namba za chini ya kizibo, itawapa fursa muhimu watanzania kujivunia utalii wao,"alisema Pamela.

Aidha Pamela alisema, baada ya kumalizika kwa droo ya shindano hilo Disemba 18, washindi wataenda kutembelea hifadhi hiyo Januari mwakani huku wao Ndovu wakigharimia malazi, chakula pamoja na usafiri na kuwataka watanzania kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo kwa kuandika namba chini ya kizibo kwenda namba 15499 au katika mtandao wa www.ndovuspecialmalt.com.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.