Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. |
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma amesema kwa sasa madalali wanaweza kutangaza nyumba, viwanja na magari yaliyoko sokoni kupitia mtandao wa kampuni hiyo bila malipo yoyote.
Akifafanua zaidi Lemma alisema dalali anayependa kupata huduma hiyo anatakiwa kufika katika ofisi za Lamudi Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam (Garden Road) na kujaza fomu ambayo itaelezea huduma yake na kuanza kuitangaza kwenye tovuti www.lamudi.co.tz bila malipo yoyote. “…Kimsingi huduma hii inawasaidia sana madalali kutangaza kazi walizonazo, bei zao na hata eneo ilipo. Mfano kama ni nyumba au kiwanja baada ya dalali kutoa taarifa za kutosha sisi tunamtangazia bure kazi hiyo kupitia tovuti yetu (www.lamudi.co.tz),” alisema Lemma.
Alisema mbali ya kuwasaidia madalali kutangaza bidhaa zao wameanza kutoa pia mafunzo ya kuwajengea uwezo madalali kuweza kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi ili kujenga heshima ya kazi zao. “Wakati mwingine tumekuwa tukifanya kazi ya kuchukua baadhi ya madalali na kuwajengea uwezo, kuwapa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi na masuala mengine ya msingi katika shughuli zao,” alifafanua Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.
Pamoja na hao alisema kwa sasa kampuni ya Lamudi Tanzania imezinduwa huduma mpya ya kumwezesha mteja kupata taarifa za uuzaji au ukodishaji nyumba ama viwanja kupitia simu za mkononi hivyo kumrahisishia kupata taarifa kwa wakati. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.