Wananchi wa
jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo zinaweza kusababisha kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.
Hayo yamesemwa
na Mbunge wa Jimbo la hilo Dotto Biteko
wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya
Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua
changamoto walizo nazo.
Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile
hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.
"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe wazazi mshirikiane na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .
Hata hivyo
ameongezea kuwa kwa vijana wameanza
kutenga asilimia kumi ya mapato na
tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo
na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja
kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.
Pia
amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na
kuwaambia kama
wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa
ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao
waliwaomba kura wakati wa kampeni.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.