Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zilizoshiriki uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma. (Picha na Mpiga Picha Wetu, Dodoma).
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akipiga penati kuashiria uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma. (Picha na Mpiga Picha Wetu, Dodoma).
Vifaa vya michezo.
* Wanafunzi zaidi ya elfu 20 kutoka sekondari wahudhuria
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Kiu ya wanafunzi na wadau wa michezi nchini kote kuhusiana na mashindano ya michezo na sanaa kwa shule za sekondari nchini imekatwa rasmi siku ya jana, baada ya kufanyika uzinduzi wa michuano hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Akifungua michuano hiyo kwa mkoa wa Dodoma,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo alitoa pongezi kwa mchango wa kampuni ya Coca-Cola kuendeleza michezo mashuleni, huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri kote nchini kuhakikisha kuwa wanatenga viwanja vya michezo.
Vile vile, aliwaelekeza maafisa elimu ngazi ya tarafa, kata, wilaya, mikoa pamoja na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha kuwa vipindi vya michezo mashuleni vinaimarishwa na kutumika kwa ajili ya shughuli za michezo na si kufundisha masomo mengine.
“Mtoto anayekosa kushiriki michezo, hata akili yake huweza kufubaa. Michezo hujenga na kuimarisha afyaya mwili na akili, upendo, ushirikiano na uzalendo”, alisema Jaffo.
Aidha, aliongeza kuwa wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na makaibu tawala wa mikoa kuhakikisha kuwa kila shule ina viwanja vya michezo vyenye vipimo sahihi na kusimamia sharia ya elimu inayotaka shule inaposajiliwa lazima kuwa na eneo la viwanja vya michezo.
Ofisi ya Rais Tamisemi haitowaangusha walimu wote wa michezo nchini katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa michuano hii, mwakilishi wa kampuni ya Coca-Cola nchini, Pamela Lugenge aliwahakikishia washiriki kuwakampuni hiyo itaendelea na dhamira yake ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbalimbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa udhamini wa michuano ya Copa-UMISSETA.
“Dhamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI ni endelevu, tukiwa tumejidhatiti kuhakikisha tunaendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi”, alisema Pamela.
Mbali na hayo, aliongeza kuwa “Pamoja na kuwepo changamoto ndogondogo za hapa na pale, tutaendelea kufanya kazi bega kwa bega na washirika wetu serikalini, pamoja na wadau wengine wote wa michezo nchini, ili kwa pamoja tuweze kufanikisha na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana”.
Alimalizia kwa kuwahakikishia wadau wa michezo nchini ya kwamba kwa mwaka huu kampuni ya Coca-Cola imejipanga kwa dhati, kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu zinazoshiriki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.