Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola
amesaini dikrii inayoruhusu tarehe 23 Agosti mwaka huu kuwa siku ya
kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.
Taarifa iliyotangazwa na idhaa ya serikali hapo jana imesema
kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Agosti 23, ambapo Dos Santos anatazamiwa
kuachia ngazi baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa karibu miongo minne.Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Dos Santos ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Kiafrika yenye utajiri wa mafuta ghafi atasalia kuwa kinara wa chama tawala cha MPLA
Itakumbukwa kuwa, chama tawala nchini Angola cha MPLA mwezi Disemba mwaka jana kilimchagua Joao Lourenco mwenye umri wa miaka 63 kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho.
Jose dos Santos aliye na umri wa miaka 74 ni kiongozi wa pili barani Afrika aliyesalia madarakani kwa muda mrefu zaidi, na mwezi Februari mwaka huu alisema kuwa hatagombea tena kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.