Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa Februari 20 mwaka huu na kuwekwa kwenye tovuti yake, ilisema majina hayo yanatoka kwenye vyuo 52 ambavyo uhakiki wa wanafunzi wake umekamilika na kwamba wanafunzi hao wanatakiwa kuthibitisha sifa zao kabla ya 28 Februari, 2017.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, wanafunzi ambao hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na tume hiyo na hivyo kukosa sifa za uanafunzi.
CBE
Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema, alisema wao walipelekewa taarifa na TCU kwamba kunatakiwa kufanyika kwa uhakiki wa wanafunzi wao na miezi miwili iliyopita wakaandaa taarifa hizo na kuziwasilisha kwao.
Alisema alishangaa kuona idadi ya wanafunzi 476 kuambiwa kuwa hawana sifa, jambo ambalo alisema ni la kushangaza.
Alisema ni makosa kusema wanafunzi hao hawana sifa wakati wanakidhi vigezo, huku akisema kuwa hali hiyo inatilia shaka.
“Yani ni hivi wewe umeniletea wanafunzi na nimewapokea halafu tena unasema huwatambui. Hayo ni makosa yao nafikiri katika kuhakiki mambo yao kwa ufasaha ,’’alisema Profesa Mjema .
Alisema taarifa zao wanazo miezi miwili iliyopita na hakuna hata mwanafunzi mwenye matatizo katika hayo majina waliyoyataja huku akihoji na kushangaa kuwa sijui imekuwaje.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Taaluma, Prof. Frolence Luoga, alisema chuo chake hakina tatizo na kwamba wanatoa elimu kwa kiwango cha ubora unaotakiwa.
Alisema wanaprogramu zilizothibitishwa na TCU na wanafunzi wao wamedahiliwa na kuthibitishwa pamoja na kufanyiwa ukaguzi, hivyo ameishangaa TCU kuja na taarifa hiyo.
Alisema lakini kuna wanafunzi ambao walidahiliwa pia siku za nyuma mfumo wa udahili haukuwa wa kupitia TCU na kabla hawajaanza udahili wa pamoja waombaji walikuwa wakifika chuoni hapo moja kwa moja wakitokea kidato cha sita na wengine vyuoni moja kwa moja na kujiunga .
Alisema wanafunzi wengine pia waliingia vyuoni hapo kwa kutumia program maalum ambazo zilikuwepo zaidi ya miaka 40 iliyopita.
SAUT
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Dk. Padre Thadeus Mukamwa, kilichotajiwa wanafunzi wake 1,046 kukosa sifa amesema huo ni uonevu mkubwa na kuharibiana sifa za vyuo.
Alisema TCU ina sheria zake na kabla ya kuwatangaza wanafunzi hao walitakiwa kuweka bayana kwamba wamekosa wao kwa kuwa udahili wote umefanywa na wao wenyewe.
Alisema walikuwa na utaratibu hata kabla majina hayo hayajapitishwa na TCU wanakutana wakuu wote wa vyuo vyote nchini, Dar es Salaam, wanafanya mkutano wa pamoja na majadiliano kwa kuangalia historia ya vyuo vyao nakisha kudahili wanafunzi.
JEMBE FM Kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA imezungumza na Afisa Habari wa Chuo Cha SAUT Living Komu na hapa anajibu swali kwanini watu wasikilaumu chuo hicho kwa kuchukuwa wanafunzi wasio na sifa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Na hapa anatoa rai kwa wanafunzi walioainishwa majina yao wakitajwa kuwa hawana sifa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
.
Kwa mujibu wa Dr. Mukamwa anasema kuwa walipata taarifa kutoka TCU wakiambiwa vigezo vya wanafunzi hao ni questionable kwa kudai kuwa namba za wanafunzi hao hazieleweki wengine kuonyesha walisoma nje.
Alisema inawashangaza kwa kuwa TCU ndio wanaofanya utaratibu wote na hata kwa kupokea kiasi cha shilingi 50,000 kutoka kwa wanafunzi hao kwa ajili ya uhakiki.
“Sasa sijui fedha walizokuwa wakipokea ilikuwa rushwa au laa na kama waliwapitisha wanafunzi hao walitoa rushwa kwanini walipokea fedha hizo,” alisema.
Alisema kuna wanafunzi wengine tayari wamemaliza kama kuna matatizo walitakiwa kuwa wanasema na kufanyiwa marekebisho lakini si kuwaambia kuwa hawana vigezo.
“TCU inakusanya data sasa wanashindwa kufanya uhakiki matokeo yao wanaharibu sifa za vyuo, kutoa lawama , wanaharibu muda wa wanafunzi ,fedha za mikopo pia,” alisema.
Alisema chuo hata siku moja hakitoi mikopo ni wao bodi ya mikopo ambao baada ya kuona wanastahili waliamua kuwapa mikopo hiyo leo kusema hawana sifa hawaoni kwamba wanaharibu sifa za vyuo na kuwachanganya wanafunzi bila kujali na wao ni binadamu pia.
Akizungumzia kauli za wakuu wa vyuo hivyo, Ofisa Habari wa TCU, Erdward Mkaku, alisema hakuna mahali wamesema kuwa wanafunzi hawana sifa bali tangazo limesema kwamba zoezi la uhakiki wa sifa limekamilika.
“Hakuna mahali tumesema wanafunzi hawana sifa, tangazo letu linasema zoezi la uhakiki limekamilika na kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa nazo,’’ alisema.
Alisema orodha yote iliwasilishwa vyuo husika na kwamba kilichobakia sasa ni kwamba watakaojiona waende kwa kiongozi wao wa taluuma wa chuo chake kwa uhakiki .
Ofisa huyo alisema TCU inafanya kazi ya kuhakiki, lakini vyuo ndivyo vinavyodahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.