Wajumbe wakikao wakifatilia.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Wananchi Mkoani Geita,wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa watafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kwa mwaka 2016 ambao watafika kwenye maeneo 12 ambayo yamepangwa kufanyiwa utafiti.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa Mkutano wa wadau wa utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwa ya mwaka 2016 uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa alisema kiwango cha maambukizi kuwa kwasasa maambukizi yamepungua kwa asilimia mbili hali ambayo imesaidia kuhifanya Tanzania kuonekana kuwa chini katika ukanda wa jangwa la sahara.
“Kiwango cha maambukizo ya VVU katika tafiti zilizopita kinaonekana kupungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011. Taarifa hii inaonyesha kuwa juhudi hizo za Serikali zimeiwezesha Tanzania kupunguza kiwango cha maambukizo ya VVU kwa asilimia mbili na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizo kati ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambapo nchini nyingi za ukanda huu zina kiwango cha maambukizo cha zaidi ya asilimia 10”Alisema Kyunga
Kwa upande wake afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba ameelezea kuwa katika mikoa ambayo wamepita wamepata ushirikiano wa mwitiko mkubwa kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wakiwafikia kwaajili ya shughuli ya upimaji.
“Kiukweli mikoa ambayo tumepita kwaajili ya zoezi hili tumepata ushirikiano mkubwa sana changamoto hazikosekani tulikutana na changamoto baadhi ya watu ambao walikuwa wameandikishwa kukosekana kwenye makazi yao kwa maana ya kwamba wameama makazi"Alisema Bupamba.
Pamoja na hayo utafiti huo utasaidia kukusanya taarifa za upatikanaji na utumiaji wa huduma zitolewazo katika kudhibiti maambukizo ya VVU na Ukimwi na vile vya tabia hatarishi vinavyochangia maambukizo ya VVU.
Utafiti wa namna hiyo ni wa awamu ya nne kufanyika nchini ,unaoangalia zaidi maswala ya afya ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004,wa pili ulifanyika 2007/2008 na utafiti wa tatu ulifanyika 2011/2012
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.