ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 17, 2012

KATIBU w' CHADEMA ANAYEDAIWA KUMNG'OA SIKIO MWANANCHI AMPA SIKU 14 MKUU WA MKOA WA MWANZA KUMTAKASA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kijana Lazaro Nolbert siku alipotinga ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikiro (anayemchunguza) na pembeni ni mama wa kijana huyo.
Katibu wa Chama cha demokrasia na maendeleo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Abel Mwesa amempa siku 14 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikiro kumwomba radhi kupitia vyombo vya habari kwa madai ya kumdhalilisha kwa kusema kuwa ndiye aliyemng'ata na kumwondosha sikio la kulia mkazi wa jijini Mwanza Lazaro Nolbert.

Abel mwesa amesema iwapo mkuu wa mkoa hatofanya hivyo kwa muda uliotajwa atamfungulia mashitaka ya udhalilishaji. Tarehe 14 kijana Lazaro Robert alifika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza kutoa taarifa za kung'atwa na kiongozi huyo wa CHADEMA akililaumu jeshi la polisi kushindwa kumtia nguvuni mtuhumiwa. Kutokana na madai hayo mkuu wa mkoa wa Mwanza alitoa agizo kwa polisi kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye aliwekwa rumande kwa siku 2
Kijana Lazaro Nolbert siku akihojiwa na waandishi wa habari.
Nae Lazaro Norbet amesisitiza kufanyiwa kitendo hicho na katibu huyo wa CHADEMA wilaya ya Ilemela akisema kuwa maelezo yake ya awali yalitofautianana na kumtaja mtu mwingine kutokana na mikwara aliyopigwa kwamba iwapo atamtaja katibu huyo kuhusika basi chamoto atakiona.

Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Mwanza Saimon Mangelepaa
Katika hatua nyingine akizungumza na vyombo vya habari jana katika ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Katibu wa siasa Itikadi na Uenezi Bw. Saimon Mangelepaa amesema kuwa CCM imesikitishwa na kitendo cha kiongozi wa juu (KATIBU) wa Wilaya ya Ilemela cha kujichukulia sheria mkononi na kumfanyia kitendo cha unyama kijana Nolbert kitendo ambacho hakina budi kulaaniwa na wananchi bila kujali tofauti za kisiasa zilizopo kwa vile ni kitendo cha kinyama kwa jamii na kimeonyesha kiongozi huyo hatambui wajibu wake kwa kuvunja sheria na kujichukulia uamuzi wake binafisi ambao umemsababishia kijana huyu ulemavu wa kudumu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.