ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 18, 2012

MBONI SHOW KUANZA KURUKA NDANI YA EATV MEI 31, 2012

Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba kinachotarajiwa kuruka hivi karibuni katika sresheni ya EATV akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kipindi chake. Pembeni yake ni msimamizi wa kipindi hicho Bw. George Tyson na msimamizi wa vipindi vya EATV. Kipindi hichi cha Mboni Show dhima yake ni kuburudisha, kuelimisha, kufundisha, uonya, uadhibu na kuelekeza jamii ya Watanzania inayokabiliwa na changamoto nyingi katika maisha ya kila siku. Na pia kipindi kinakusudia kuleta mapinduzi makubwa katika muendelezo wa vipindi vya mahojiano.

Msimamizi wa kipindi cha Mboni Show Bw. George Tyson akielezea ubora wa kipindi hicho.

Meneja wa Vipindi kutoka EATV akizungumza katika uzinduzi huo wa kipindi cha Mboni Show kinachotarajiwa kuanza kuruka Mei 31 ndani ya EATV.

Waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba akiteta jambo na msimamizi wa Vipindi wa EATV. Lakini pia anapenda muziki, mitindo na ni mjasiliamali anayemiliki kampuni yake binafsi iitwayo 'CHOCLATE PRINCES' ambayo inaendesha duka la mavazi, vipondozi na viatu vya kike lakini pia ndiyo waandaaji wa kipindi kipya cha luninga 'THE MBONI SHOW'. Picha zote na www.kajunason.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.