ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 4, 2013

MEYA WA JIJI AONGOZA WASHIRIKI WA REDS MISS NYAMAGANA KUFANYA USAFI JIJINI MWANZA

Ni sehemu tu ya nyuso za warembo wanaowania taji la unyange wa Miss Nyamagana 2013 walioshirikiana na Mstahiki Meya  wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (CCM) kufanya usafi wa mazingira katika Mtaa wa Rufiji Wilayani Nyamagana Jijini hapa

MSTAHKI Meya  wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula akizoa taka katika zoezi la usafi aliloshirikiana na washiriki wa kinyang’anyiro Reds Miss Nyamagana mwaka 2013. 

Warembo wakifanya usafi wa kina kwenye matundu madogo ya maji katika barabara ya mtaa wa Rufiji jijini Mwanza. 


Mtangazaji wa Star Tv na kiss Fm Yvonna (kushoto) akishirikiana na warembo washiriki wa kinyang’anyiro Reds Miss Nyamagana mwaka 2013 kufanya usafi wa mazingira katika Mtaa wa Rufiji Wilayani Nyamagana Jijini hapa

Usafi haukuishia barabarani tu bali pia ulizigusa hata kaya zilizopo pembezoni mwa barabara hiyo kama mfano safi wa kuigwa katika utunzaji mazingira.

Barabara iling'aa kwani takataka zote iwe makopo, mchanga au hata karatasi ndogo kama vocha havikusalimika kubakia barabarani.

Usafi kwa pamoja ukiendelea.

Wenye maduka nao walipata somo.

Usafi makini

Mratibu wa shindano la Reds Miss Nyamagana Mc. Stopper wa Stopper Entertainment (katikati) pia mkono wake ulitumika.

Wakikusanya taka ni diwani wa kata husika (kulia) pamoja na meya, Yvonna aliyeshika toroli  na mrembo akizoa taka. 

Kona hdi kona hapa ilikuwa kona kuelekea soko la jumapili.

Mmoja wa warembo wa kuelekea kinyang'anyiro cha Miss nyamagana akizibua matundu madogo ya maji barabara ya Rufiji.

Usafi hadi miferejini.

"Msiache taka" says Mtahiki Meya Mabula kwa warembo.


MSTAHKI Meya  wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (CCM) ameongoza washiriki wa kinyang’anyiro Reds Miss Nyamagana mwaka 2013 kufanya usafi wa mazingira katika Mtaa wa Rufiji Wilayani Nyamagana Jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika mataa wa Rufiji ambako usfi ulikuwa ukifanyika Mstahiki Meya Mabula alisema kwamba usafi uliofanywa na warembo hao ni sehemu ya huduma ya usafi kwa jamii  inayowazunguka.

Alisema kuwa usafi wa mazingira katika jiji la Mwanza ni mpango endelevu ambapo hivi karibuni Halmashauri ya jiji inataraji kuzindua wiki ya usafi itakayowashirikisha wananchi na wadau mbalimbali ili kuendelea kudumisha ushindi wa Tuzo ya usafi na mazingira inayoshikiliwa kwa mara ya saba sasa mfululizo.

Meya alisema kwamba Wiki ya usafi na mazingira imepangwa kuzinduliwa rasimi Mei 15 mwaka huu itakayokuwa na mkakati mpya ulioboreshwa kutokana na changamoto zilizopo na zilizoonekana kupitia shughuli za usafi wa kila siku ambapo watendaji wake wamezibaini

“Warembo hawa kufanya usafi leo ni kuongeza chachu kwa wananchi kuona kwamba jukumu la usafi ni la kila mtu, kwani jamii imekuwa na imani potofu kuwa wafanyao usafi ni watu wa hali ya chini, hivyo kwa hatua hii iliyochukuliwa na warembo hawa itakuwa mfano tosha kwa jamii kubadilika”

Mstahiki Mabula pia aliipongeza Kamati ya Miss Nyamagana kupitia Kampuni ya Stopper Entertainment inayoanda mshinano hilo na kutoa wito kwa waandaaji wengine kuiga mfano huo na kuzingatia changamoto na kulenga changamoto ya usafi ili Jiji la Mwanza liendelee kutetea sifa na Tuzo ya usafi kwa kipindi kingine.

Naye mmoja wa wa warembo wanaoshiriki shindano hilo Rose Peter akiwawakilisha wenzake alisema kwamba kufanya usafi mbele ya jamii imawaongezea kujiamini na kwao wameona thamani na umuhimu wa wao kushiriki mashindano kama hayo kwani jamii katika barabara mbalimbali na maeneo waliyokuwa wakifanya usafi imelipokea zoezi hilokwa taswira chanya iliyoamsha ari kwa jamii kushiriki kila siku kutunza mazingira. 

Picha ya pamoja na Mstahiki Meya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.