ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 5, 2013

ELIMU FC NDIYO MABINGWA ESTER BULAYA CUP 2013

 



Na Shomari Binda,
         Bunda

MICHUANO ya Kombe la Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana (CCM) Esther Bulaya inayojulikana kama Esther Bulaya Cup imemalizika wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo Timu inayoundwa na Wadau wa Elimu wilayani hapo Elimu Fc iliibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa Mwaka 2013.

Mashindano hayo ambayo yalizikutanisha timu zaidi ya 30 kutoka wilayani Bunda ilimaliza kwa kuzikutanisha timu za Bunda Sport Club na Elimu Fc, ambapo iliibuka bingwa wa Kombe hilo kwa Mwaka 2013 kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 3-1 baada ya kufungana bao 1-1 ndani ya dk 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni moja pamoja na Kombe.

Mshindi wa Pili alipata zawadi ya Shilingi laki Tano huku mshindi wa tatu timu ya Town Star waliokuwa mabingwa watetezi ilijipatia kiasi cha shilingi laki tatu pamoja na seti ya jezi baada ya kuifunga timu ya Majengo fc katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

Akiongea wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali kwa Washindi,Mbunge Esther Bulaya alisema kuna baadhi ya watu ambao wanapanga Mikakati ya kuhujumu Mashindano hayo yasifanyike na kudai kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa wa Michuano hiyo katika kukuza vipaji vyao.

Alisema lengo lake kuanzisha mashindano hayo ikiwa ni msimu wa wake wa tatu ni kuhakikisha vipaji vilivyopo Wilayani Bunda  vinaendelezwa na wale watakaobahatika kufanya vizuri wanatafutiwa timu za kufanyia majaribio ili kuweza kuwaendeleza.

“Mimi nashangaa sana kuna baadhi ya watu wanataka kuhujumu Mashindano haya kitu ambacho hawatawatendea haki vijana wa Bunda maana ndiyo walengwa,napenda kuwaahidi Vijana wenzangu nitaendelea kudhamini mpaka mwisho wa ubunge wangu na hata kama sitokuwepo kwenye hii nafasi nitayadhamini Mpaka kufa Kwangu”.

"Watu wanataka kuweka itikadi ya kisiasa kupitia mashindano haya,mimi sipo huko wakati wa michezo tufanye michezo na wakati wa siasa tufanye siasa na niko tayari kushirikiana na mtu yoyote katika kutaka kuboresha zaidi mashindano haya pale atakaponijia.

"Ukitaka kuona mashindano haya hayapo kisiasa nimekwishatoa vifaa na kuandaa mashindano kama haya katika Wilaya nyingine za mkoa wa Mara kwa maana mimi ni Mbunge wa vijana kutoka mkoa mzima,"alisema Bulaya.


Aidha baadhi ya Wadau wa Michezo Wilayani Bunda walimpongeza Mbunge huyo na kusema  Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Bunda huku wakimuomba kuiendeleza Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka mitatu iliyopita.

Walisema wilaya ya Bunda ni mmoja ya wilaya Mkoani Mara ambayo iilikuwa nyuma katika suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa wilaya hiyo imeonekana kuwa kinala na kudaiwa kuzipiku Wilaya nyingine ambazo apo awali zilikuwa mbale.

“Unajua hii wilaya ilikuwa nyuma sana Kimichezo lakini tangu huyu Mbunge ameanzisha haya Mashindano sasa hivi Bunda inaongoza kwa Michezo hasa Soka maana hata bingwa wa Mkoa na mshindi wa pili wanatoka Bunda sasa hayo si Mafanikio”? alisema Juma Mbano mkazi wa Manyamanyama.

Michuano hiyo ya Esther Bulaya Cup 2013 iliunganisha Michezo mbalimbali ikiwemo Michezo ya bao,draft pamoja na Pool table,ambapo na kila mchezo zawadi mbambali zilitolewa na kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 12 kwa mwaka huu

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.