Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mlezi wa Aflewo (Africa Let’s Worship) Askofu Fredy Kyara, alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwani hakuna kiingilio. Alisema kuwa, tamasha hilo
litashirikisha kwaya mbalimbali kutoka makanisa 32 ya madhehebu tofauti katika kusifu na kuabudu.
Askofu kyara alisema, tamasha hilo linafanyika kwa mara ya tatu tangia kuanzishwa hapa nchini mwaka 2011 na kuenea nchi zote za Afrika. “Tamasha hili limeboreshwa kwa kuongeza muiondombinu ya utendaji kazi, kwa kutanua wigo wa ushirikishwaji wa makanisa mengi,” alisema Kyara.
Aidha matasha mengine ya Aflewo, yanatarajia kufanyika nchi nzima kwa kufanyika kila mkoa, kwa mwaka huu litaanza kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Moshi na Zanzibar na hatimaye Afrika yote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.