ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 6, 2012

KUANZA KWA SAFARI ZA TRENI HIYO KESHO UNAFUU KWA WANANCHI NA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA

Wakati kesho (TEREHE 7/12/2012) Treni ya abiria inataraji kuanza upya safari yake kutoka jijini Dar es salaam hadi jijini Mwanza ikiwa ni kutekeleza kwa ahadi ya serikali kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi  Dr. Harson Mwakyembe aliyoitoa Bungeni wakati wa kupitishwa bajeti ya wizara yake.
 Jijini mwanza blogu hii imeshuhudia mafundi pamoja na vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi sehemu mbalimbali ikiwemo zile za kupumzikia abiria  huku pia abiria wakiendelea kukata tiketi zao kwa ajili ya safari ya kwanza tangu kusitishwa takribani miaka mitano siku ya jumapili.


 Kuanza kwa usafiri huo kumerejesha matumaini kwa wananchi wanaotumia usafiri huo hasa kwa wafanyabiashara wanaosafiri na kusafirisha bidhaa kwa wingi kila kukicha kutokana na gharama zake kuwa nafuu zaidi ikilinganishwa na ile ya mabasi ya abiria ya kutoka Mwanza hadi jijini Dar es salaam. 

Bofya Play kusikiliza..


 Hata hivyo changamoto imejitokeza kwa abiria watakao tumia usafiri huo wa treni kwani sasa watalazimika kuwa na vitambulisho au hati za kusafiria, kitambulisho cha mpiga kura au barua ya mwenyekiti wa mtaa anapotoka abiria huyo ili kusaidia kuweka kumbukumbu sahihi kwa abiria waliosafiri kwa siku husika kutambulika pindi  ajali au tatizo lolote linapotokea.
 Njia za treni na mafundi wake.


Mafundi.

Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.

Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.


Mafundi wapaka rangi wakilikarabati eneo la kuketi abiria  katika maandalizi ya mwisho. 



Nao wadau wa usafirishaji barabarani kwa pikipiki maarufu kama bodaboda nao tayari wameanza kujongea eneo hili ambalo si muda mrefu litarejea kwenye shamrashamra zake kama siku za nyuma ilikuwa mishemishe mchana hadi usiku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.