ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 7, 2012

MEYA AONGOZA HARAMBEE YA WANAFUNZI MWANZA KUMCHANGIA KIJANA MWENYE TATIZO LA KIBOFU

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni mchango wake kwa kijana Dickson Wasiwasi ambaye blogu hii hivi karibuni ilitoa taarifa zake za kushindikana kufanyiwa upasuaji hapa nchini, akihitaji kiasi cha shilingi milioni 20 kwaajili ya kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Shughuli hii imefanyika jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba ikiandaliwa na kamati ya Bunge la Watoto  jijini Mwanza na kuwashirikisha wanafunzi wa Sekondari toka shule mbalimbali.

Timu B.

Timu A.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akifanya ukaguzi kwa timu A.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akifanya ukaguzi kwa timu B.

Timu A na timu B zikipepetana ndani ya dimba la CCM Kirumba katika mchezo wa hisani kunogesha Harambee hiyo waliyoiandaa kumchangia kijana Dickson Wasiwasi, ambaye ametumikia zaidi ya oparesheni tatu kwenye hospitali ya Rufaa Bugando bila mafanikio na sasa ni juhudi kumpeleka nchini India ambako inaaminika kuna wataalamu waliobobea zaidi watakao msaidia.

Sehemu ya wanafunzi waliojitokeza.

Bunge la Watoto jijini Mwanza likipata picha ya pamoja na Mstahiki Meya, Kamishna wa Chama cha ADC Bw. Ituji, baba na kijana Dickson.

Ambapo wito umetolewa kwa Mashirika, Makampuni, Watu binafsi, Vikundi kujitokeza kumchangia kijana huyu ili akapate matibabu, huu ukiwa ni mwanzo tu wa harakati za vijana hawa wenye mapenzi mema wasiopenda kuona kijana mwenzao akitaabika na kunyanyapaliwa.
 DICKSON VEDASTUS WASIWASI ALIZALIWA 7/07/1996 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA, KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE (KIKIONEKANA WAZIWAZI), MADAKTARI WAMEMFANYIA MATIBABU KUPITIA OPARESHENI MARA TATU BILA MAFANIKIO. ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 20, NAYE HANA UWEZO HIVYO AMEOMBA WASAMALIA WEMA KUMSAIDIA KUNUSURU ADHA NA MATESO AYAPATAYO MTOTO WAKE.

 CHANGIA KUPITIA AKAUNTI ZIFUATAZO:-
CRDB     0152457709500
AZANIA 003003005102370001

SIMU 0762324527 OR 0683580004

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. wadau hili ni bunge la wanafunzi shule za sekondari..sio bunge la watoto kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na vyombo vya habari..naomba kuwasahihisha!!..ni mimi spika wa bunge la wanafunzi...charles francis marwa.. you may get me through 0752 20 20 52

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.