ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 25, 2022

RC PWANI AFUNGA MICHUANO YA UMISHUMTA.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akibabidhi kombe kwa Baadhi ya timu ambazo zimefanya vizuri katika michuano hiyo.

Na Victor Masangu, Pwani

MKUU wa mkoa Pwani Abubakari  Kunenge amewataka wanamichezo wa Umitashumta Mkoa wa Pwani watakaokwenda kushiriki katika kivumbi Cha  michezo ya Umitashumta kitaifa mkoani Tabora kuhakikisha wanaupeperusha vema Mkoa na sio kufanya vinginevyo.


 Kunenge ametasema  hayo leo katika mashindano ya ufungwaji wa Umitashumta Mkoa Pwani yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani hapa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wanafunzi kutoka wilaya zote Saba za Mkoa wa Pwani.


 Aidha mkuu huyo amesema kwamba wanamichezo watakaoenda Tabora hasa wasichana wajiepushe na vitendo vyote vichafu kwani wakifanya hivyo watajiletea aibu wao wenyewe, wazazi wao na Mkoa Pwani kwa ujumla.


 'Kikubwa zaidi nawataka wanamichezo wote wa Mkoa wa Pwani mtakaochaguliwa kutuwakilisha Mkoa nendeni mkapamnane na mkashindane na mrudi na ushindi mkubwa na si kwenda kujiingiza kwenye mambo yote machafu", 


    "Kwa jinsi mlivyojiandaa kuanzia leo nitakuwa mlezi wa timu hii ila kikubwa nasisitiza nidhamu pindi mtakapokuwa uko katika michuano hasa nyie wanamichezo ambao no waluvana wavulana nendeni mkawalinde madada zenu,"akisema KUNENGE.


Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa huyo ameuomba uongozi wa Mkoa kupitia kwa Katibu Tawala kukaa na kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuinua michezo mkoani Pwani.


   "Tumeweza kukaa na kuboresha elimu tukapata wawekezaji na sasa ni zamu ya kuona ni namna gani tutaweza kwenye michezo", alimaliza Kunenge


Kwa upande wake Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta alisema kuwa lengo kubwa kwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanaibuka kidedea katika michuano ya Taifa katika kushinda katika michezo mbali mbali.


Aidha Buleta aliwaomba wadau na viongozi mbali mbali kushirikiana bega kwa bega kuisapoti timu ya Mkoa kwa Hali na Mali ili kuwawezesha wachezaji wote kuwa na molali ya kuibuka na ushindi katika kivumbi Cha michuano hiyo ngazi ya Taifa.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.