ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 10, 2023

NMB YAZINDUA UMEBIMA?

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB - Martine Massawe wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Umebima kwa Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa, Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB - Martine Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na  Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar- Naima Said Shaame katika picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni ya bima, mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Umebima visiwani Zanzibar.

 Wananchi viziwani Zanzibar wakiendelea kupata huduma mbalimbali baada ya uzinduzi wa kampeni ya Umebima.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Umebima visiwani Zanzibar.


Benki ya NMB ikiwa wasambazaji wa bidhaa mbalimbali za makampuni 10 ya bima, wamezindua rasmi kampeni ya 'Umebima - Teleza na Hii!' visiwani Zanzibar itakayowawezesha kutoa elimu na kuhamasisha mauzo ya bima mbalimbali zikiwemo za: Majanga, afya, moto, machinga, maisha, vikundi, vyombo vya moto, nyumba, biashara, kilimo, usafirishaji na kadhalika, zitakazosaidia kutoa fidia endapo majanga yatatokea.


Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wetu wa Idara ya Bima wa NMB - Martine Massawe, huku Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na Meneja wa Biashara wa NMB Zanzibar - Naima Said Shaame wakishuhudia.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  Bw.  Idrissa Kitwana Mustafa aliwaasa wananchi kuchukua juhudi ya kuzielewa aina zitolewazo za bima, ili waweze kukata kwani ni kwa manufaa yao ya sasa na hata baadae.


Lakini pia, aliiipongeza NMB kwa ubunifu wa kampeni hii ambayo ni fursa nzuri ya maendeleo.


Aidha,  Mkuu wa Idara ya Bima wa benki hiyo, Bw. Martine Massawe, alisema timu ya NMB itakua mitaa mbalimbali visiwani Zanzibar kwa mwezi mzima kuhakisha wanatoa elimu ya bima na wanananchi wanaelewa ili waweze kuchagua ni ipi wanaihitaji. Bima hizi, mteja wa NMB na asiyekua mteja anaweza kuzinunua kutoka kwa matawi ya benki hiyo yaliyotapakaa nchi nzima.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.