ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 6, 2023

POLISI SHINYANGA WAKAMATA WATU 9 TUHUMA ZA UJAMBAZI.

 

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watu tisa wanaosadikiwa kuhusika katika tukio la ujambazi lililotokea Februari 4, 2023 katika kambi ya Wachina wanaojenga reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR eneo la Old-Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga.


Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kufuatia msako na doria zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Magomi amesemna pamoja na watuhumiwa hao jeshi hilo limekamata pesa za kigeni za nchi mbalimbali ambapo amesema uchunguzi unaendelea na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Kamanda Magomi ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutojihusisha na hujuma dhidi ya mradi wa reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR pamoja na uhalifu mwingine.

Kamnada huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga amesema kuhujumu miundombinu katika mradi wa SGR na miradi mingine ni kurudisha nyuma juhudi za serikali ambayo imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.