
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wazamiaji 12 kutoka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku huu mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini ili kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna mili iliyokwama kwenye Meli ya MV Spice Islander iliyozama chini ya bahari eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi wiki iliyopita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Aboud Mohammed, amesema kuwa wazamiaji hao wamewasili wakiwa na zana za kisasa za uzamiaji na kwamba kazi ya kwanza itakayofanywa na timu hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaifikia meli hiyo iliyozama umbali wa karibu nusu kimometa kwenye mkondo mkubwa wa maji na majabali.


Tangu kuokolewa kwa abiria 619 na kuopolewa kwa miili ya watu 197 hadi jana jioni, hakujapatikana mtu hai ama mwili wa abiria aliyekufa maji ukielea juu ya maji ama kukokotwa kupelekwa mwambao mwa nchi kavu.
Katika eneo ilipo Meli hiyo zipo Meli nyingine za MV Kasa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na MV Mamba ya Jeshi la Polisi ambazo zote ziliwasili alfajiri siku iliyotokea tukio hilo la kuzam,a kwa MV Spice Islander.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.