TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mrusi wa
Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali. Wawili hao walikuwa
wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble on the Mountain” na ulikuwa
ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz ambaye
atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24 Juni
mwaka huu.
Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi
mojawapo zikiwa The Santorini Blue, Perfect Strangers, The Big Fight na
nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenz ataingia mjini Moshi akitokea nyumbani
kwake New York , Marekani terehe 21 Juni tayari kikimbia mbio hizo za Mt.
Kilimanjaro Marathon.
Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye
anajulikana kama “Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa
tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara
ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika
baada ya bondia mmojawapo kuingia mitini kwa woga.
Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake
Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza
kuifikia.
Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika
Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa
Ngumi Duniani (WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye
kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa
wa hali ya juu.
Hata hivyo Rashid Matumla amepangiwa kupigana
na bondia mwingine siku za usoni ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi
huyo!
Imetolewa na:
Onesmo A.M.Ngowi
President IBF/USBA for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Director, BRAND-Africa
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education & Resources Network (iEARN) to Tanzania
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education & Resources Network (iEARN) to Tanzania
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.