Nashauri sana ndugu zangu tunaojumuika katika vinywaji vyenye chachu hatuna haja kukimbilia vinywaji vya asili visivyo na viwango vinavyoweza kuchakachua afya zetu, kuna kinywaji safi toka TBL kilicho thibitishwa na shirika la viwango TBS. Kileo kinaitwa NZAGAMBA kina kilevi asilimia 4.5%, ujazo lita 1, viambata maji, unga wa mahindi meupe, mtama mwekundu na tindikali ya chakula. bei ni shilingi za madafu 700/= tu! PIGA ZAKO 3 'baridi' BIASHARA 'kwishni' KAMA ULAYA VILE.
Kipitashoto kikuu cha Wilaya ya Sengerema.
Utalii wa ndani kwa ndani.
Daraja kutoka kijiji cha Issena kuelekea kitongoji cha mtakuja wilayani Sengerema limekuwepo tangu Uhuru wa Tanganyika.
Msimu wa sikukuu hapa na msimu wa matunda hapa! pichani ni magunia ya maembe njiani wilayani Sengerema. Bei kwa gunia sijui sikumkuta mwenye mali kwani yalikuwa kama yametelekezwa hivi.. Unaambiwa hayaibiwi ingawa hakuna ulinzi.
'Msimu wa sikukuu ndo huu' hata kama kwa wengine imekuwa kama chai kuipata asubuhi, Tamaduni za Kitaani kwetu aka 'uswazi' ziko pale pale! na hazikamiliki bila kupiga mnuso. Pichani mzee Ismail wa Imalaseko supermarket Mwanza akipanga viroba vya mchele kwa oda ya mteja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.