Makabidhiano hayo ambayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Nyumbani Hotel mjini Mwanza yalianza kwa maelezo mafupi kutoka kwa meneja mpango wa baraza la Habari Tanzania Bi. Pili Mtambalike ambaye aligusia matatizo yaliyochangia kukwamisha harakati kadhaa za maendeleo ya chama kwa kipindi kilichopita.
PILI MTAMBALIKE MENEJA PROGRAM WA MCT.
Meneja huyo ameyataja matatizo hayo kuwa ni tatizo la fedha kwa wanachama kutolipa ada kwa muda muafaka, waandishi kukosa weledi wa majukumu yao na migongano ya kiuongozi kati ya waandishi na waandishi.
RAIS WA UTPC KENNETH SIMBAYA AKIONESHA NYENZO ALIZO KABIDHIWA.
Rais wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Bwana. Keneth Simbaya amesema kuwa jukumu kubwa walilonalo wanachama ni kujenga umoja endelevu kwa waandishi wa habari nchini kwa kila wanachama kufanya kazi kwa ufanisi na kiwango cha hali ya juu hivyo kuleta taswira ambayo jamii inahitaji kufikia kimaendeleo
Naye katibu mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga ameyataja mambo yanayodhamiriwa kufanyika ndani ya mpango huo wa makabidhiano kuwa ni kuweka misingi ya kidemokrasia katk utawala, kuweka mifumo ya menejimenti ya bodi, vilevile kuweka kanuni za utendaji wa bodi ili kutoa fursa kwa kila mwanachama aweze kutenda kazi kwa mujibu wa kanuni.
WANACHAMA WA UTPC MKUTANONI.Kulia ni mwenyekiti chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma bw. Juma Nyumayo ambaye vilevile ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili UTPC akiwa bize' mkutanoni.
KUTOKA KUSHOTO WALIOKETI NI;John Nguya (meneja wa fedha MCT), Zilipa Joseph (makamu wa rais), Pili Mtambalike (meneja programu), kajubi Mukanga (katibu mtendaji MCT), Kenneth Simbaya (rais UTPC)na Jackob Kambili (kaimu mkurugenzi mtendaji wa UTPC-MWANZA). Waliosimama ni bodi ya UTPC.
Katika miaka sita ya uongozi wake kwa waandishi, Baraza la habari Tanzania (MCT) linajivunia kuwa na uwakilishi wa vyama vya waandishi wa habari kwa kila mkoa nchini, vyama vyenye kuweza kuweza kujiendesha vyenyewe na hatimaye leo Baraza hilo linakabidhi mradi kwa klabu za waandishi wenyewe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.