ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 25, 2010

BENKI YA FBME TAWI LA MWANZA YATOA ZAWADI YA X-MASS KWA KITUO CHA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU MWANZA.

Katika kuitikia wito wa Clouds fm (X-MASS ZAWADI)wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuwawezesha kutabasamu hasa katika kipindi kama hiki cha kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa masia Yesu Kristo, Benki yako ya FBME kupitia tawi lake la Mwanza jana jioni imetoa zawadi ya krismasi na mwaka mpya kwa kituo cha watoto wanaoishi mazingira magumu cha 'Back Home Upendo Daima' kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Afisa wa FBME BANK bwana Alawi Mdee akikabidhi sabuni kwa mlezi wa kituo cha 'Back Home Upendo Daima' Sister Monica.

Marry X-mass; Zawadi za mchele, mafuta, sabuni, chumvi, unga, sukari, unga wa ngano yaaaani....Ni tabasamu tu na vicheko kwa watoto!....AKSANTE FBME BANK!!!

Chakufurahisha Watoto hawa wamefundishwa kusaidiana na kuishi kwa upendo wa kumjua mungu, hivyo kila wanachokifanya wanafanya pamoja wakisaidiana kama ndugu wa tumbo moja.

Wadau wa FBME BANK walipata pia fursa ya kutembelea vyumba wanapolala watoto hao.

Ni vitanda vya juu na chini twaita Double deka vyenye kutosha watoto wote 30 wa kituo hiki, kila mtoto na kitanda chake. Nawapa shavu uongozi wa kituo hiki kwa kuwa na mazingira mazuri yenye kuzingatia usafi kama wa nyumbani kwa baba na mama.

Kuishi kunahitaji misingi bora na kanuni, si kwa mkubwa tu bali hata kwa mdogo.

Mama mlezi wa kituo hiki Anna Malima, akitoa maelezo jinsi watoto wanavyoishi na malezi kwa wadau wa FBME tawi la Mwanza.

Mlezi wa wa kituo cha 'Back Home Upendo Daima' sister Monica ametoa shukurani kwa benki ya FBME kwa msaada huo wa zawadi ya X-mass kwani ni nafasi inayowafanya watoto kama hao wajisikie vyema zaidi na kujiona nao ni sehemu katika jamii, aidha amewataka watu na mashirika mengine kuiga mfano huo wa FBME kwani watoto kama hao ni Watoto wetu sisi sote.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.