ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 22, 2013

YALIVYOKUWA MAZISHI YA GABRIEL ANDERSON MUNISSI HII LEO.














Marehemu Gabriel Anderson Munissi aliyefariki dunia tarehe 19 Nov 2013 amezikwa leo Nkokashi Masama wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro ambapo ndugu jamaa na marafiki aliofanya kazi nao enzi za uhai wake walisafiri toka pande mbalimbali hapa nchini wakiwemo wengi wadau kutoka jiji la Mwanza, kuhudhuria mazishi hayo yaliyokuwa yamegubikwa simanzi kubwa.

Gabriel alifariki dunia mara baada ya kujifyatulia risasi kichwani ikiwa ni kabla ya kufanya mauaji kwa watu wawili na kujeruhi wengine watatu wawili kati yao wakiwa taabani na kisha baadaye (jana) mmoja kati ya hao walio kuwa taabani (niki maanisha majeruhi Fransis Shumira) alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Kufariki dunia kwa Francis kuna fanya idadi ya watu waliofariki dunia katika tukio hilo hadi sasa kufikia wanne (akiwemo gabriel) huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred Newa ambaye ni mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.

Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar es salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na klabu ya wazee na maziko yakisubiri kutengemaa kwa afya ya mama mzazi.

Familia imekiri binti yao Christina na Marehemu Munisi kuwa walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahikumfanyia siku za nyuma.

Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa mfanyakazi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar, wakati Shumira ni Baharia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.