ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 23, 2024

RFO PWANI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA WANAHABARI WA PWANI




NA VICTOR MASANGU,PWANI 

Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Pwani mrakibu Mwandamizi Jenifa Shirima  ametoa elimu kwa waandishi  habari wa Mkoa wa Pwani kuhusiana na masuala mbali mbali ya kuandika habari zinazohusiana na  kujikinga na majanga  mbali mbali ya moto.

Kamanda Shirima ameyasema hayo wakati aliposhiriki halfa ya  maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ngazi ya Mkoa wa Pwani ambayo yamefanyika leo Mei 23 mwaka huu katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Kamanda Shirima alisema kwamba waandishi wa habari ni kiungo kikubwa  katika kuelimisha jamii juu ya kuweza  kukabiliana na majanga ya moto.

Aliongeza kuwa kama Jeshi la zima moto  wataendelea kutoa elimu katika makundi mbali mbali ikiwemo kundi la waandishi wa habari lengo ikiwa ni kuandika habari za kuwaelimisha wananchi kuhusiana na jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.
 


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.