Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud
Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud
Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud
Mgimwa akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud
Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda
Na Fredy Mgunda,Mufindi.
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud
Mgimwa amekabidhi jumla ya mifuko ya saruji 400
na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi
pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya
wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza wakati
wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la
kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma
yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.
“Nimetoa jumla ya mifuko
ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa
madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea
kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi
Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa
halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa
kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za
kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya
halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.
“mimi lengo langu
inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na
kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya
wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna
kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi
Kaskazini” alisema Mgimwa
Aidha Mgimwa
alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji
cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni
kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mgimwa amewapongeza
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya
kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi
Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.
Obedi Madembo,
Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti
wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya
ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.
“Hata ukiangalia
mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi
kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia
wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya
kata ya Mapanda
Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda
Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga
mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa
kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.
“Wananchi kweli wananjitoa sana
kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu
kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye
shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na
wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa
elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa
wananchi wote” alisema Kalenga
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.