ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 22, 2014

FLAVIANA MATATA, AY WASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 18 AJALI YA MV BUKOBA JIJINI MWANZA.

JANA ilitimia miaka 18 tangu ndugu zetu walipopata ajali na Meli ya MV. Bukoba 21 May 1996, na wengi kupoteza maisha! Ni tukio kubwa lililoua mamia ya watu na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania.
Miss Universe tanzania 2007 na mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata jana alijumuika na wananchi wengine wa mkoa wa Mwanza katika ibada maalum ya kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya waliopoteza maisha yao baada ya ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba yapata miaka 18 sasa.
Flaviana Matata (mwenye gauni la bluu kulia) akiwa amesindikizana na jamaa, ndugu na marafiki akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mama yake mzazi aliyefariki kupitia ajali hiyo.
Akiwa ameambatana pia na mwanamuziki wa kimataifa Ambwene Yesaya 'AY' (mwenye kofia nyeusi), mwanamitindo Flaviana Matata alishirikiana na wadau hao pamoja na wananchi wengine kuwasha mishumaa kama sehemu ya ibada kwa marehemu hao walio fariki dunia yapata miaka 18 sasa.
"Tutawakumbuka daima"
Ajali ya kuzama kwa Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamotarehe 21/05/1996 nakupoteza maisha ya zaidi ya watu 1000.
Mwanamuziki wa kimataifa Ambwene Yesaya 'AY' (mwenye kofia nyeusi kulia) ni mmoja kati ya marafiki waliofika eneo hili la makaburi ya waliokufa katika ajali ya Mv Bukoba, na kushiriki ibada maalum ya kuwaombea wote walio tangulia mbele za haki. 
Misa hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa dini, ndugu wa karibu wa Flaviana akiwemo baba yake mzazi, marafiki zake wanamchi mbalimbali na pia viongozi wa Serikali, na viongozi na wafanyakazi wa Marine Services Co. LTD. 
Ni tukio kubwa lililoua mamia ya watu na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania, nayo miili ya watu kwa mamia imelala hapa. Eh Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema twakuomba uwarehemu watu wako.
Amen.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.