VYA
HABARI LEO TAREHE 14.01.2017
·
MWANAMKE
MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMPIGA MTOTO WAKE HADI
KUFARIKI DUNIA WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA
TAREHE 11.01.2017 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA NSUMBA KATA YA
KISEKE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULIKANA
KWA JINA LA JOYCE MATHAYO MIAKA 33, MKAZI WA MTAA WA NSUMBA, ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMPIGA FIMBO MTOTO WAKE AITWAYE MATHAYO MANIS
MIAKA 12, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI
KUFARIKI DUNIA KWA KOSA LA UTORO SHULENI KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA
KUWA SIKU YA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAREHEMU ALIMKATALIA MAMA YAKE KWENDA SHULE
AKIDAI KUWA YEYE HATAKI TENA SHULE, NDIPO MAMA YAKE ALIPATWA NA HASIRA NA
KUAMUA KUMPA ADHABU YA KUMCHAPA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE, NDIPO GHAFLA
ALIBADILIKA HALI YAKE YA AFYA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MCHACHE BAADAE, WANANCHI
WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA MAPEMA ENEO LA
TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/ WALEZI AKIWATAKA WAWALEE WATOTO WAO KATIKA MAADILI MEMA NA NIDHAMU HUKU
WAKIWAELIMISHA MAMBO MAZURI NI YAPI NA MABAYA, ILI KUEPUSHA ADHABU ZA VIPIGO
KWA MTOTO PINDI ANAPOKOSEA ZITAKAZO PELEKEA MAJERA AU VIFO KAMA TUKIO HILI
LILILOTOKEA KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
·
WATU
WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA UHALIFU WA NJIA YA
MTANDAO WILAYANI ILEMELA
MNAMO TAREHE 11.01.2017
MAJIRA YA 17:00HRS JIONI KATIKA HOTELI IITWAYO KINGDOM HOTEL ILIYOPO ENEO LA
KONA YA BWIRU WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU WANAWAKE WAWILI NA
MWANAUME MMOJA WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1. EVELIN SILYVESTER MIAKA 39 MKAZI
WA TABATA DAR ES SALAAM, MRANGI, 2.BEATRICE MATABA, MIAKA 36, MKEREWE MKAZI WA
TABATA DAR ES SALAAM, NA 3.FITINA MILCHAEDES MIAKA 42, MUHA, MWANAMUME NA MKAZI
WA BUSERESERE MKOANI GEITA, WOTE WAFANYA BIASHARA, WANASHIKILIA NA JESHI LA
POLISI KWA KOSA LA KUFANYA UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTOA HUNDI HEWA KWA
WAFANYABIASHARA WENYE MADUKA MAKUBWA NA MAKAMPUNI HAPA JIJINI MWANZA KITENDO
AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI POLISI WALIPOKEA
TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA JUU YA UWEPO WA WATU HAPA JIJINI MWANZA WANAOFANYA
UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTOA HUNDI HEWA KWA WAFANYA BIASHARA WENYE
MADUKA MAKUBWA NA MAKAMPUNI NA KUCHUKUA BIDHAA ZAO KISHA KUZIHIFADHI KATIKA
STOO YAO NA BAADAE KUZIUZA.
ASKARI WALIFANYA
UPELELEZI KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUWAKATA WATUHUMIWA WOTE
WATATU KATIKA HOTELI TAJWA HAPO JUU, AIDHA KATIKA MAHOJIANO NA ASKARI WATUHUMIWA
WALIKIRI KUHUSIKA KATIKA UHALIFU HUO WA MTANDAO KISHA WAKAWAPELEKA ASKARI KWEYE
STOO ZAO ZILIZOPO MAENEO YA NYAMANORO WILAYANI IELEMELA AMBAPO ZILIKUTWA BIDHAA
MBALIMBALI AMBAZO NI MABATI BUNDLE 20 ZA GEJI 30 YENYE THAMANI YA TSH
9,600,000/=, KATONI 75 ZA SABUNI YA UNGA AINA YA KLEED YENYE THAMANI YA TSH
6,200,000/=, PAMOJA NA MAFUTA YA KUJIPAKA AMBAYO THAMANI YAKE BADO
HAIJAFAHAMIKA.
POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI
ILI KUPATA MTANDAO WA WAHALIFU HAWA LAKINI PIA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA AMBAO
TAYARI WAMEKAMATWA KWANI UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA WATUHUMIWA WAMEFANYA
UHALIFU WA AINA KAMA HII MKOANI GEITA, MOROGORO NA MAENEO MENGINE, PINDI
UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA
KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI
NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI
WAHALIFU WAWEZE KUKAMTWA MAPEMA KABLA MADHARA MAKUBWA HAYAJATOKEA KWA WANANCHI,
LAKINI PIA ANAWATAKA WAMILIKI WA NYUMBA ZA WAGENI KUTOA TAARIFA POLISI PINDI
WANAPOPOKEA WAGENI AMBAO WANAWATILIA MASHAKA. AIDHA ANAWAKUMBUSHA WAFANYA BIASHARA
KUWA MAKINI NA WAHALIFU WA AINA KAMA HII AMBAO WAMEJITOKEZA KATIKA MKOA WETU WA
MWANZA.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.