ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 14, 2017

"ULIZENI TENA KWANINI NILIMKABIDHI BENDERA DIAMOND" WAZIRI NAPE

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye January 11, 2017 alimkabidhi nyota wa Afro Pop, Diamond Platnumz bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa mashindano ya Africa Cup of Nation (AFCON) iliyofunguliwa Januari 14, 2017 nchini Garbon hivi karibuni.
Waziri Nape alisema haya siku ya kumkabidhi Diamond bendera ya taifa:

“Siku ya leo nina furaha  kumuaga ndugu yetu Diamond na kundi lake amabapo wamepata fursa ya kuipeperusha bendera ya nchi yetu kwa dunia nzima.

“Kama nilivyosema kuwa AFCON ni mashindano makubwa na yanaangaliwa na dunia nzima kwa hiyo kwa tukio hili inaonyesha ni jinsi gani sanaa yetu ya Tanzania imekuwa kubwa ndio maana leo nipo hapa kwa niaaba ya Serikali kumpongeza Diamond na kumkabidhi bendera ya Tanzania.‘” alisema Nape.
Wakati pazia la michuano hiyo likifunguliwa, ufunguzi huo uliambana na burudani kabambe ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa Afrika na nje ya Afrika. Diamond alitumbuiza kuiwakilisha nchi huku akiwa amevalia sare na wacheza shoo wake iliyoandaliwa kwa rangi za bendera ya taifa.

Baada ya uzinduzi huo kufanyika Waziri Nape ameandika haya katika mtandoa wa ‘Twitter’

“Ulizeni Tena Kwanini Nilimkabidhi Bendera Diamond”aliandika Waziri Nape



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.