Idadi ya wabunge wa chama cha Democrats cha Marekani waliotangaza kususia sherehe za kuapishwa Donald Trump kama Rais mpya wa nchi hiyo inazidi kuongezeka.
Baada ya Donald Trump kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliogubikwa na malalamiko na kasoro nyingi huko Marekani, upinzani dhidi ya mwanasiasa huyo asiyeficha chuki zake za kibaguzi dhidi ya watu mbalimbali wakiwemo Waislamu unazidi kuongezeka siku hadi siku.
Sherehe za kuapishwa rais huyo mteule wa Marekani zinatarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu wa Januari yaani siku tano zijazo. Idadi ya wabunge wa chama cha Democrats wanaotangaza kususia sherehe hizo inaongezeka, suala ambalo linazidi kuonesha mizozo na mivutano iliyotanda baina ya wafuasi wa vyama viwili vya Democrats na Republican huko Marekani.Maandamano dhidi ya Donald Trump nchini Marekani |
Huku hayo yakiripotiwa, wapinzani wa Donald Trump wameanzisha kampeni ya wiki ya malalamiko ya umma itakayoendelea hadi wakati wa kuapishwa rais huyo mteule wa Marekani.
Maelfu kadhaa ya wananchi wa Marekani jana walianzisha kampeni hiyo mjini Washington kwa kaulimbiu inayosema, pasipo uadilifu hapana amani. Waandamanaji hao wameshiriki kwa wingi kwenye maandamano hayo licha ya kunyesha mvua na baridi kali.
Waliozungumza kwenye maandamano hayo ya ufunguzi wamelaani matamshi ya chuki na udhalilishaji ya Donald Trump dhidi ya makundi ya watu wachache na wanawake pamoja na hatua yake ya kupinga mradi wa huduma za afya ulioanzishwa na Barack Obama, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.