MCHOMVU. B12. DJ FETTY. |
WATANGAZAJI wa kipindi Double XXL cha Radio Clouds fm 88.5 Dar, Adam Mchomvu, Dj Fetty na B12 ni ubishani wa 'KIUTANI' ulioanza hatimaye wakazichapa wakiwa LIVE On Air.
Linapokuja suala la 'Talk Talk za Mastori', Mchomvu dizaini ni kama ana utata utata siku zote uliojaa 'MASIHARA' lakini jana alim challenge 'SIRIAZ' Fetty kuhusu deal ya kurelease Compilation Album ambayo anaifukuzia.
Wakati huo huo b12 akawachallenge kuwa wamechelewa sana coz yeye tayari ameshaiandaa China na soon inakuja, wakati huo huo Adam hakupenda hicho kitu, akasema ilikuwa ni AIDIA yake na ataitoa yeye ndipo Fetty na b12 wakamchana alishindwa kutoa Album tangu mwaka jana kipindi cha Fiesta hii ataiwezea wapi...!!!? Ndipo Adam akaja juu kwa jibu la Fetty (akiwa amepanik dizain) na kutaka kumchapa makofi Fetty.
B12 katikati akijaribu kurescue situation, ni.aibu coz yote yalikua on Air na b12 mara kwa mara alijaribu kuzima mic kabla ya ugomvi na wenzake wakazidi kumuona kuwa anabana na mbona ni suala la ufafanuzi kama mara zote wanavyofanya (UWAZI NA UKWELI) lakini haikuwa salama na ilikuwa sahihi.
KILICHOFUATA:-
Kilichofuata ni sokomoko la ndondi hali iliyo sababisha hali ya studio kuchafuka huku baadhi ya vitendea kazi muhimu vikivunjwa na kusababisha kipindi kilichokuwa kikifuata cha jahazi kuanza kwakusuasua kikikosa baadhi ya viashiria kutokana na Kompyuta ya matirio muhimu kuvunjwa....
HEKA HEKA:-
Mara baada ya kusumbuliwa na SMS nyingi za wasikilizaji kuwa 'mara zote Clouds fm inazungumza habari za watu wengine leo tunataka hekaheka zenu' hivyo leo kupitia kipindi cha LEO TENA kinachoendeshwa na Da-Hu katika segment ya Hekaheka Geha Habibu amelazimika kuwatafuta kwa njia ya simu Ma-prizenta hao ambao inasemekana wamepigwa barua nzito huku wakitakiwa kuandika barua za kujieleza kwa uongozi. SIKILIZA KWA KUBOFYA PLAY.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.