ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 4, 2014

VIJANA WA NYAMONGO WILAYANI TARIME MKOANI MARA WAIKUBALI SEMINA YA FURSA.

Muelimishaji wa Semina ya Fursa mhitimu wa Chuo Kikuu ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip hop nchini kutoka kundi la Weusi akizungumza na vijana wa kata ya Ingwe, Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara jinsi ya kuzibaini na kuzifanyia kazi fursa zilizopo katika mazingira yao. 
Kaimu Meneja Mahusiano wa North Mara Gold Mine Bwana Zakayo Kabelo aliwaasa washiriki hao wa Semina ya Fursa kusikiliza kwa makini yale yote yatakayo jadiliwa, kuyazingatia kwaajili ya kwenda kuyafanyia kazi. "Furaha yetu kama mgodi pamoja na Radio Clouds itatimia pale tutakapotoka hapa na baadaye kukutana na vijana waliotoka humu wakiwa katika maisha ya ustawi tofauti na walivyokuwa siku za nyuma"
Muelimishaji wa Semina ya Fursa mhitimu wa Chuo Kikuu ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip hop nchini kutoka kundi la Weusi akizungumza na vijana wa kijiji cha Ingwe, Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara jinsi ya kuzibaini na kuzifanyia kazi fursa zilizopo katika mazingira yao. 
Muelimishaji wa Semina ya Fursa mhitimu wa Chuo Kikuu ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Hip hop nchini kutoka kundi la Weusi, akiweka mkazo katika moja ya mada zilizo wasilishwa ambapo mada ya kwanza ilikuwa ni
1. Maana ya Fursa na Utazitambuaje Fursa na utawezaje kuzitumia ili upate tija katika maendeleo.
2.Utawezaje kujenga tabia ya kufanikiwa na kupata maendeleo.
3.Nidhamu ya matumizi ya fedha.
4.Ujasiliamali wenye tija. (kuna wajasiliamali wengi lakini hakuna tija watu wanafanya shughuli zao za uwekezaji kwa kubahatisha bila malengo wala mpango mkakati, ubunifu na kadhalika)
5.Ushiriki mzuri katika jamii (Unawezaje kuwa kaka bora, mama bora na baba bora)
Afisa Ushirikishwaji (ABG) Nicodemus Keraryo akizungumza na wanasemina.
Kikundi cha sanaa kata ya Ingwe, Nyamongo, ambacho kimejikita katika kutoa elimu kupitia burudani kikitoa burudani kwa washiriki wa semina ya Fursa.
Mmoja kati ya akinamama ambao ni washiriki wa Semina ya Fursa katika kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime akishiriki katikakuuliza maswali.
Vijana nao walikuwa mstari wa mbele.
Akina dada na akina mama wameitikia wito kushiriki Fursa.
Uwasilishaji wa mawazo pamoja na maswali muhimu ndani ya Semina ya Fursa.
Kwa umakiiiiini Seminani.
Akinamama nao wamo! Walilitumia vyema jukwaa la Fursa kuelezea vikwazo vinavywakabili ndani ya jamii zao hali inayosababisha wao kushindwa kupata kufaidi Fursa zinazo wazunguka.
Muelimishaji wa Semina ya Fursa Bi. Rehema yeye alizungumzia Umuhimu wa kufanya kazi  huku ukiwa na Afya bora na jinsi ya kuboresha Afya likiwemo suala la kuzingatia Tiba bora na sahihi.
Washiriki seminani.
"Afya ikiwa mgogoro jamii itazorota kimaendeleo, uzalishaji utapugua, na jamii itarudi nyuma kwani hata akiba yote itaelekezwa kwenye matibabu badala ya kuelekezwa kwenye masuala ya maendeleo likiwemo suala la kulipia  ada za shule kwa watoto, kununua pembejeo na zana muhimu za kilimo na mambo kadha muhimu" alisema Rehema.
Diwani wa viti maalum kata ya Kemambu, Tarafa ya Ingwe, Nyamongo wilayani Tarime Mh. Mwajuma Issa Chacha akichangia ndani ya Semina ya Fursa.
Elimu na daftari...
Wazee walijichanganya na vijana kuipata Elimu ya Fursa.
1. Unawezaje kujua kuwa wewe ni mzuri wa kitu fulani na unakimudu?
2. Je umewahi kujiuliza watu wa jamii yako wanakutizamaje na wanakupa thamani gani?
3. Vipi uwezo na mapungufu yako? Ukichukuwa muda wa kutafakari majibu ya yote haya utagundua kuwa wewe unamapugufu gani na una sifa gani, mwisho wa siku utakacho baini basi kifanyie kazi.
Semina ya siku ya kwanza ilimalizika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.