ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 31, 2019

HAZINA YAKABIDHIWA KILO 324.96 ZA DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 27 NA FEDHA TASLIMU MILIONI 305



Kilo 325 ya dhahabu, fedha taslimu Sh305 milioni na magari mawili yaliyotaifishwa na Mahakama baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa na kusafirisha dhahabu kinyume cha sheria imekabidhiwa Hazina.


Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.



Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.


`



Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni Dhahabu kilo 324.96 yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 27, Fedha taslimu shilingi milioni 305, Mzani wa kupimia ubora wa madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi Januari mwaka huu wilayani Sengerema. Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa Serikalini baada ya kutaifishwa pia.


Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.