ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 30, 2019

SERIKALI YANUSURU ANGUKO LA BEI YA PAMBA


MWANZA. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ana imani kuwa ununuzi wa zao la pamba utaanza mara moja kwa bei ya sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo. Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya bei kwa takriban ya wiki nne tangu bei elekezi ilipotangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga kwamba bei hiyo ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019.

Alikuwa akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao cha dharura kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Kilimo na Viwanda, Makatibu Wakuu wa Kilimo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na  Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Wengine ni wawakilishi wa Wabunge wa mikoa hiyo, Makatibu Tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya zote za mikoa hiyo, na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hizo. Pia kilihudhuriwa na wanunuzi wa pamba, wakulima na maafisa wa benki kadhaa.

Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali bado inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuwakutanisha wadau wa mazao ya kibiashara ili yaweze kuwa na tija kwa wakulima. Alisema kazi hiyo inafanywa wa Wizara ya Kilimo. Mazao hayo ni pamba, chai, kahawa, korosho, tumbaku na chikichi.

Pia alisema Bodi ya Pamba iachiwe jukumu la kutoa leseni za ununuzi wa zao hilo na kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wakifanya kazi hiyo waache mara moja.

Mwenyeji wa Kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akiongoza utaratibu wa uwasilishaji mijadala kwa wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini hapa.
Mfanyabishara mkongwe Mzee Christopher Mwita Gachuma akiwakilisha maoni ya wafanyabishara katika kusanyiko hilo la wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini
Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicha cha dharura....
Kuhusu ubora wa pamba, Waziri Mkuu alitaka wananchi waelimishwe ili waache kuweka maji au mchanga kwenye pamba kwa minajili ya kuongeza uzito kwani kwa kufanya hivyo wanachafua jina la Tanzania pindi inapopelekwa kuuzwa nje ya nchi.
Pia alitaka vyama vikuu vya ushirika vijiridhishe kuhusu ubora wa maghala ya kuhifadhia pamba kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia wakulima wauze mapema pamba yao mara baada ya kuivuna.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.