Watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc) wametakiwa kutokuwa na mapumziko siku ya kesho badala yake waende sokoni, madukani na magengeni kufuatilia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ameyaswema hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya Temeke kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala kuhusu utekelezaji wa katazo hilo.
Utekelezaji katazo la mifuko ya plastiki limeanza leo baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza Bungeni kutangaza ifikapo Juni mosi mifuko ya plastiki haitakiwi kutumia na kosa kuingiza, kusambaza, kuzalisha na kuiuza.
Kabla ya kuzungumza na wananchi hao, Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli alifanya ziara ya kutembelea eneo la Kariakoo na kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali kuhusu matumizi ya mifuko mbadala.
"Mtanisamehe sana kesho hakutakuwa na mapumziko wala sherehe baada jambo hili kuonyesha mafanikio. Msione kazi imeisha mambo ndio kwanza yameenza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.