Mwandishi wa Habari Joseph Gandye kutoka Watetezi TV" |
Anaandika Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Dotto Emmanuel Bulendu.
Jioni ya leo baada ya ratiba ngumu,nimekutana na habari ya kukamatwa na kuendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa mwandishi wa Habari Joseph Gandye kutoka Watetezi TV".kwa kile kinachodaiwa kuandaa stori ya TV inayodaiwa kukiuka sheria(Jeshi la Polisi ndiyo linamshikilia).
Gandye alikwenda mkoani Njombe kufanya stori ya TV juu ya tuhuma za unyanyasaji walizofanyiwa vijana na baadhi ya Askari na wakuu wa kiwanda walichokuwa wakifanyia kazi.
Nimeamua kuitafuta stori na kuipata,nimeiona nawe waweza itazama(nimekuwekea link-https://youtu.be/0LhQMsHSFWo)
Maoni yangu.
Stori hiyo haina tatizo lolote la kisheria,kiweledi na kitaaluma bali inachangamoto ya kimaadili kwa sehemu ndogo ambayo sidhani kama inaweza kuwa ni jinai.
Kwa nini nasema haya?
1.Stori imehusisha vyanzo vyote viwili,chanzo kitu (physical source) na chanzo mtu(human source)
2.Stori imebalansi uzania wa vyanzo kwa kuhusisha vyanzo vitatu kutoka chanzo mtu kwa maana ya mlalamikaji na mtuhumiwa,maana aliyelalamika yumo,aliyelalamikiwa pia yumo kwenye stori.
3.Stori imezingatia msingi mkuu haki za binadamu (haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa),kwani mwandishi ameweza kutoa nafasi kwa Uongozi wa kiwanda pamoja na Jeshi la Polisi(ambao ni watuhumiwa)waweze kujibu tuhuma hizo maana RPC katumika kwenye stori na kiongozi wa kiwanda).
Udhaifu upo wapi?
Binafsi nauona udhaifu kwenye eneo la maadili baada ya mwandishi kuacha baadhi ya maneno ambayo yana ukakasi kidogo kutumika maana kwenye uandishi tunaambiwa tujitahidi kupunguza ukali wa maneno (ila siyo sheria ni suala la maadili).
MSIMAMO WANGU.
Jeshi la Polisi muachieni Joseph Gandye maana amefanya stori kwa kuzingatia misingi ya Habari ni nini?na amezingatia misingi yote ya kisheria ya matakwa ya uandaaji wa Habari.Katumia vyanzo vyote vinavyotakiwa.Kuendelea kumshikilia Gandye ni kuendeleza kile kinachohisiwa kuwa kuna ubinywaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari na waandishi wa Habari.
Wasalaaam
Bulendu E.D
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.