ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 10, 2019

HISTORIA YA MAISHA YA HAWA NTAREJEA


Maisha ni mzunguko, Changamoto ni daraja la mafanikio, Mipango sio matumizi, Mvumilivu hula mbivu na Penya nia pana njia.  usilo lijua ni kama usiku wagiza!.  Karibu kwenye Historia ya 'Hawa Ntarejea'.

Majina yake kamili anaitwa Hawa Said lakini jina la usanii anaitambulika kama 'Hawa Ntarejea' Mnamo mwaka 1990 ilipofika tarehe 5/2 ndipo Hawa alipo zaliwa na kuanza kuishi maisha ya hapa Duniani. Kipindi hicho hakuweza kutambua kama Dunia inaweza kugeuka na kuwa chungu, kutokana na umri wake ulikuwa bado.  Kadri siku zilivyo zidi kwenda Hawa alizidi kukua na kuanza kujitambua. 

Bahati nzuri Mungu alimjaalia Hawa kipawa cha Sauti nzuri na uwezo wa kuitumia, hivyo ulipofika wakati Hawa akajitambua vizuri ndipo alipoanza kuusogelea Muziki.  Jamii ilimpokea kwa kishondo mara baada ya kushirikishwa kwenye wimbo wa Ntarejea na Diamond Platnumz, ambapo kila mmoja  alitambua Hawa ninani!  Kwenye wimbo alitoa sauti nyororo iliyo jaa simanzi kutokana na Ujumbe wa Wimbo huo.

Hivyo basi umaarufu wa wimbo huo ndio uliyo pelekea mpaka leo anaitwa Hawa Ntarejea.  Mbali na mahusiano ya kimuziki baina ya Hawa na Diamond Platnuz wawili hao walikuwa katiaka Mahusiano ya Kimapenzi. Na hata kabla ya kuimba pamoja walikuwa tayari ni marafiki.

Baada ya maisha ya muziki wa Ntarejea Hawa na Diamond Platnumz waliendelea kuishi kama mtu na Mpenzi wake, lakini tunakumbushwa tu kuwa hakuna marefu yasio na ncha,  Hivyo Penzi la Hawa na Diamond halikuweza kudumu.  Amini nakwambia upendo ukizidi kiasi huleta madhara, Hawa alikuwa na upendo uliyo pitiliza kwa Diamond Platnumz hali hiyo ilipelekea akawa na wivu uliopita kiasi mwisho Penzi likaangamia.

Pamoja na hayo yote msimamo wa Hawa katika ndoto zake ili kuwa ni kuja kuwa msanii mkubwa Duniani kote! Tukirejea kwenye utangulizi wangu hapo awali kuna msemo nimesema “Mipango sio matumizi” kumbe basi kuna vitu ambavyo vilibadilisha na kuharibu mtazamo wa ndoto za Hawa. Baada muda kidogo miaka ya 2015 -2016  Hawa alipata mwanaume wa kumuoa na ndoa ikafungwa  kutokana na tofauti zao za kidini Hawa alilazimika kubadili jina akaitwa 'Angel' Ndoa ilifanikiwa vizuri tena ni ile ya kupendana kwenye shida na raha.

Kuna wengine wanaweza wakasema ni mikosi lakini pengine si kweli bali ni mipango tu ya Mungu,  Ndoa ya Hawa ambaye kipindi hicho alikuwa ni Angel na Mumewe haikuweza kudumu pia!. Ilikuwaje ilikuwa hivi, Maisha ya ndoa ya Hawa hayakuchukua muda mrefu,  lakini ndani ya muda huo mchache kulikuwa na mikwaruzano ya hapa na pale baina ya ndugu wa Mume kwa Hawa yalizidi kuwekwa sawa na maisha mengine yakawa yanaendelea kama kawaida.

Sikumoja Mume akamwambia Hawa kuwa anataka kusafiri kwenda kutafuta maisha, lakini Hawa hakuvutiwa saana na safari hiyo maana hakukukubaliana naye yaani alikataa, kwa kumwambia kuwa “ Mbona mimi nalizika na tunacho kipata kwani nimesema siwezi kula ugali na mlenda au matembele? Kwani huko kuna kitugani cha ziada? Maswali haya ya Hawa hayakuweza kusaidia chochote kwasababu Mume alikuwa tayari kapanga plan zake! Hivyo aliaga kuwa anaenda Botswana Baada ya safari hiyo, Mume alikata mawasiliano kabisa kwa Hawa pia ndungu wa Mume hivyo hivyo, Hawa akabaki kwenye mataa mpaka hii leo 2019 toka 2015 – 2016 hana mawasiliano yeyote na Mumewe.

Kutokana na mgongano wa matukio yote hayo katika maisha ya Hawa yalipelekea akajikuta akiishi katika ndimbwi kubwa la mawazo. Hali hiyo ikasababisha ajikite zaidi kweye vilevi hasa pombe aina ya Gongo kwa kudhani kuwa itamsaidia kuondoa mawazo kumbe ndio alizidi kujiangamiza kiafya.  Lakini pia alikondeana sana kiasi cha kupoteza mvuto kwenye macho ya watu.

2018 ulikuwa ni mwaka wa Hawa kuteseka kiafya maana alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo,  madhara ambayo yalisababishwa na  Mawazo pamoja na Vilevi ambavyo alikuwa akitumia kwa kusudio la kupunguza mawazo. Amini na kwambia Ukitenda wema utatendewa wema, pamoja na kwamba Hawa alikuwa kwenye hali mbaya lakini Diamond Platnumz alitambua thamani ya Hawa kwa roho ya  huruma  alishirikiana na team yake ya WCB   kumpeleka India kwa ajili ya Matibabu ya Moyo, Baada ya matibabu Afya ya Hawa ilirejea vyema,  Mapaka sasa   Hawa anaendelea na Muziki na mashabiki wake bado wana upendo wa dhati kwa kile anacho kifanya.

Ukirejea tena kwenye uangulizi wangu nimesema “Changamoto ni daraja la mafanikio” hivyo basi kumbe huwezi kufanikiwa pasipo kupitia changamoto mbalimbali.  Kwa mambo ambayo ameyapitia msanii Hawa yanatosha kuukaribisha ulimwengu wa Mafanikio, lakini kupitia maisha yake naamni kuna mengi utakuwa umejifunza.

Note: Hawa ni msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye alifamika kwa wimbo wa 'Ntarejea' aliyo shirikishwa na Diamond Platnumz,  lakini ananyimbo zake zingine kama Kucheka na Shagala bagala kwa yote aliyo pitia ikumbukwe tu kuwa Hawa Ntarejea anyota ya Upendo pia anakipaji kikubwa anahitaji suport ya kila mmoja ili kutimiza ndoto zake alizo ahidi tangu alivyo kuwa mdogo!.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.