ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 9, 2019

MTATURU AONYA MADIWANI NA VIONGOZI WA CHADEMA WANAOCHOCHEA WANANCHI KUTOCHANGIA MAENDELEO


NA MWANDISHI WETU, IKUNGI

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) amewaonya Viongozi na Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Katika Kata zote za Jimbo hilo kuacha tabia ya kupita katika vijiji na Kata zao kuwahamasisha wananchi na viongozi kutomuunga mkono Mbunge huyo, kutoshiri na kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo atawaumbua kwa wananchi na kuwaomba wasiwasikilize hali washirikiane naye katika maendeleo.

Mtaturu alitoa onyo hilo jana alipokuwa akihutubia mamiaa ya wananchi waliofulika kwenye mkutano wake wa hadhala uliofaanyika senta ya Kata ya Makiungu, ambapo aliwataka wananchi kuwapuuza kwa kile wanachowahamasisha kwa kuwa yeye ndo Mbunge halali wa Jimbo hilo aliyekwisha apishwa.

"Msiwasikilize na muwakatae kwa kusambaza uongo na hawawatakii mema kwani wao mliwachagua washirikiane na wananchi kuhakikisha kero za majisafi, afya, elimu, umeme na miundombinu ya barabara ikiwemo na mawasiliano ya mitandao ya simu za mkononi zilizopo katika vitongoji, vijiji na Kata zinapatiwa ufumbuzi wa haraka lakini kwa wanavyofanya ni kuwachelewesha na kusababisha miradi ya maendeleo kukwama kutekelezeka kwa kukosa Madiwani wa kuisemea Halmashauri na hata Bungeni," alisema.

Mbunge Mtaturu alisema wananchi waache ushabiki wa vyama vya siasa kwa kufananisha na ushabiki wa timu za mpira wa miguu kwa kuwa siasa ni maisha hivyo lazima wawe makini kuchagua viongozi wa watakaokuwa wawakilisha wa wananchi watakaowaunganisha katika maendeleo bila kuwabagua katika itikadi za vyama vya siasa, rangi, dini na makabila yao bali wawaunganishe kushirikiana pamoja kujiletea maendeleo.

"Mimi ndo Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa mujibu wa Katiba, Sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano hivyo hivyo wanaota ndoto kudhani kuwa tunacheza na kuigiza watambue kuwa kazi iliyopo ni kuhakikisha kero zote zinafikishwa serikalini na kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kama mnavyojua tayari Rais aliagiza na Wizara ya Maji wametupatia Sh bilioni 2 za kutekeleza mradi wa majisafi Wilaya ya Ikungi yenye majimbo mawili baada ya Mimi kutaka kuomba Bungeni baada ya kuapishwa na Spika Job Ndugai kunipa nafasi ya kuuliza swali ninyi ni mashahidi mliona," alisema.

Mbunge Mtaturu aliwaeleza wananchi hao kwamba miradi ambayo serikali haikuitekeleza kwa miaka tisa kwa kukosa mtu wa kuisemea Mbungeni sasa atahakikisha inatekelezwa ili wananchi wapate huduma bora katika sekta za Afya, Elimu, Majisafi, Umeme, Miundombinu ya barabara na mawasiliano ya mitandao ya simu sanjali na kuwa na uhakika wa pembejeo za kilimo na mifugo ili wananchi waweze kuongeza kipato cha familia na maendeleo kwa ujumla.

Mkutano huo wa Mbunge uliohudhuliwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo ambayo alionya viongozi wa vyama vya siasa wanaopita kupanga njama za kuwahamasisha wananchi kuvuruga uchaguzi wa serikali za Mitaa watakumbana na mkono wa serikali ambapo watakamatwa na kuchukuliwa hata za kisheria hivyo aliwataka wananchi kuwa watulivu nawajipange kuchagua viongozi watakaowaunganisha, kuwaongoza na kushirikiana nao katika maendeleo kwenye maeneo yao ya vitongoji na vijiji pasipo kuwabagua.

Katika Mkutano huo viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji wakiwemo wanachama wa vyama vya upinzani 40 kutoka Chadema walibwaga manyanga na kujivua uanachama na kurejesha Kadi zao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakiongozwa na Ayubu Mohamed Mwenyekiti wa Kata hiyo, baadhi ya waliokuwa makada kindakindaki wa Chadema ni Maiko Mahiki, Maiko Mathias, James Emmanuel, Gaspary Majoa, Miraji Seleman, Eliabu Aloyce, Abudallah Lessolesso, Hamisi Kinyori, Shaban Selema, Laurence Fransis, Gaza Boy, George Yunde na Maiko Ghamaa ambapo walisema wanamuunga mkono Mbunge Mtaturu kwa kupambania maendeleo ya Jimbo hilo ambapo waliomtangulia waliendekeza kuwagawa kwa itikadi za kisiasa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Makiungu ulipofanyikia mukitano huo, Hamis Haji alisema wananchi wa Kata hiyo wameteseka kwa miaka tisa bila kutekelezewa miradi ya maendeleo na mara nyingine ukosekanaji wa huduma ya majisafi ilisababisha ndoa nyingi kuvunjika huku wawakilishi wao ambao ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu kabla ya kutenguliwa na Spika na Madiwani waliendekeza na kuwachochea kubaguana na kuwazuia wananchi kuchangia miradi ya maendeleo hali iliyopelekea Jimbo hilo kudumaa kimaendeleo hivyo kumpata Mtaturu wameona ni Jembe jipya linalowapa matumaini mapya ya maendeleo na kutekelezeka kwa miradi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.