ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 7, 2019

ZAIDI YA WAKAZI MILIONI 1 6 KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA MWANZA


KAMATI ya ulinzi na usalama za wilaya mkoa wa Mwanza zimetakiwa kuhakikisha zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa linafanyika kwa ufanisi ili kutimiza azma ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaojitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura linafanyika kwa amani na utuli bila bugdha yoyote huku akionya kwa yeyote atakaye kwamisha zoezi hilo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa muujibu wa katiba ya nchi. 
Rai hiyo imetolewa mapema hii leo na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza John Mongella,  wakati akifungua kikao cha wasimamizi kamati mbalimbali za ulinzi na usalama kwa wilaya zote 7 na halmashauri zake 8.

Jeh mkoa wa Mwanza umejipanga vipi katika zoezi hilo la uandikishaji linaloanza rasmi kesho (8 -October- 2019) kwenye kata mbalimbali? 


Jeh mkoa wa Mwanza unamalengo ya kuandikisha wananchi wangapi? 


Kanuni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mtaa za mwaka 2019 nchini Tanzania zimeainisha aina nane za vitambulisho ambavyo msimamizi wa kituo cha uchaguzi anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe ili kujiridhisha na jina kama ndilo liko katika orodha ya mpiga kura.
Kanuni hizo zimetolewa tangu Agosti 23 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jafo jijini Dodoma mbele ya viongozi mbalimbali wa mikoa na wadau wa siasa.
Kanuni hizo zimetaja vitambulisho hivyo ni kitambulisho cha mpiga kura, cha kazi, hati ya kusafiria, kadi ya bima ya afya, cha shule au chuo, cha mfuko wa hifadhi ya jamii, leseni ya udereva na kitambulisho cha Taifa.
Kanuni hiyo ya 33 kifungu cha pili kinasema, "Msimamizi wa kituo anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe kitambulisho kitakachoonesha kuwa jina la mpiga kura huyo ndio lililomo kwenye orodha ya wapiga kura."

Sehemu ya wajumbe wa mkutano wa kamati ndogo na kubwa za ulinzi na Usalama toka halmashauri mbalimbali za wilaya mkoa wa Mwanza. 
Sehemu ya wajumbe.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro (kushoto) ni sehemu ya wajumbe wa mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza, Emmanuel Stenga, (kushoto) yu sehemu ya wajumbe wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa kusanyiko hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.